BAYERN MUNICH YAICHAPA TENA BARCELONA MABAO 3 KWA NUNGE






BAYERN Munich usiku huu waiadhibu Barca nyumbani na kutinga fainali ya kwanza ya Ligi ya Klabu Bingwa Ulaya ambapo sasa watakutana na Wajerumani wenzao baada ya kuichapa Barcelona 3-0 kwenye Uwanja wa Nou Camp na hivyo kusonga mbele kwa jumla ya mabao 7-0. 

Mabingwa hao wapya wa Ligi Kuu ya Ujerumani waliimaliza mechi mapema wiki iliyopita kwa ushindi wa 4-0 nchini Ujerumani na hapakuwa na namna ya kufufuka kwa Wahispania hao wakati Arjen Robben alipofunga goli la kuongoza dhidi ya kipa Victor Valdes katika dakika ya 49. 
Kudhalilika kwa Barca kulikamilishwa mwishoni mwa mechi wakati Gerard Pique alipojifunga mwenyewe na Thomas Mueller, ambaye alifunga magoli mawili katika mechi yao ya kwanza, akapachika la tatu kwa kichwa. 
Barca, kama Bayern ambao wanafukuzia taji la tano la Ulaya, wanategemea kipaji cha Lionel Messi, ambaye anarejea kutoka katika majeraha ya misuli ya nyuma ya paja na ambaye aliachwa benchi, lakini bila ya Mwanasoka Bora wa Dunia huyo hawakuwa na makali yoyote. 
Bayern watacheza dhidi ya Borussia Dortmund katika mechi ya fainali kwenye Uwanja wa Wembley mjini London Mei 25 baada ya Dortmund kuitoa Real Madrid kwa jumla ya mabao 4-3 Jumanne.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.