BREAKING NEWS.......KANISA LA KATOLIKI ARUSHA LADAIWA KULIPULIWA LEO
Kiongozi wa kanisa Katoliki ulimwenguni ,Papa Francis
............................................................................
Leo kulikuwa na uzinduzi wa Parokia mpya ya
Olasit mjini Arusha. Mgeni rasmi alikuwa Mwakilishi wa Papa toka Vatican.
Kulikuwa na wageni wengi waliambatana na mwakilishi wa papa, wakiwemo maaskofu,
mapadre na watawa kutoka mataifa mbalimbali.
Mtoto
mmoja ameeleza kuwa aliona watu waliokuwa kwenye mini bus wakirusha kitu
kuelekea kwenye mkusanyiko wa wakristo waliokuwepo kwenye ibada.
Taarifa
zinaeleza kuwa eneo kubwa limetapakaa damu, watu wengi wamejeruhiwa. Inasadikiwa
kuwa wapo waliokufa lakini haijathibitika. Muda huu vyombo vyote vya usalama
vipo eneo la tukio.
Kwa
update zaidi sikiliza Radio Maria http://streema.com/radios/play/6848.
Hivi
sasa kuna taharuki kubwa, na kuna taarifa ya milipuko mingine, haijulikani kama
ni ya washambuliaji au ya polisi, mbali na eneo la ibada.
Nawapeni pole nyingi waliokumbwa na
mkasa huu, wakatoliki, wakristo wote na wanaolitakia amani Taifa letu.
Taarifa kutoka mkoani Arusha ambazo mtandao huu wa www.matukiodaima.com umezipata zinaeleza kuwa kuna mlipuko mkubwa mfano wa bomu umejitokeza katika kanisa la RC Arusha na kujeruhi baadhi ya waumini.
Mlipuko huo unadaiwa kusababisha taharuki kubwa katika mji wa Arusha na kuendelea kuiweka nchi katika hali tete zaidi .
mwandishi maalum wa mtandao huu kutoka Arusha anasema kuwa tukio hilo limetokea katika parokia ya Olasit mjini Arusha na bado jitihada za uokoaji zinaendelea kufanyika.
Comments