DK PETER KAFUMU AWASHUKURU WANA IGUNGA KWA UVUMULIVU WAO, ATAKA MAENDELEO BILA KUJALI ITIKADI ZA VYAMA
Mbunge
wa jimbo la Igunga aliyerejeshwa na mahakama kuu Dk Peter Kafumu
akizungumza na wana Igunga mara baada ya kuwasili mjini humo leo
kuwashukuru wananchi na wapiga kura wake kwa kuwa naye bega kwa bega
katika matatizo hayo, Mkutano huo umefanyika kwenye uwanja wa Sokoine
mjini Igunga ukiongozwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa Halmashauri
kuu ya CCM Ndugu Nape Nnauye, amesema anaomba ushirikiano kwa kila mwana
Iguna bila kujali itikadi za vyama vya siasa. PICHA NA KIKOSI KAZI CHA
FULLSHANGWE- IGUNGA Mbuge
wa Jimbo la Igunga Dk Peter Kafumu akihutubia mkutano wa hadhari mjini
Igunga leo kulia ni Nape Nnauye Katibu wa Itikadi na Uenezi NEC Maelefu ya wana Igunga wakiwa katika mkutano huo leo
Maandamano ya pikipiki yakiongoza msafara wa Mbunge wa jimbo la Igunga Peter Kafumu na Nape Nnauye. Wananchi wa Igunga wakipmokea mbunge wao kwa mabango yenye ujumbe wa kumkaribisha jimboni mwake
Dk Peter Kafumu akivishwa shada la maua mara baada ya kuwasili mjini Igunga leo
Comments