EU YASAIDIA BILIONI 20 KUKUZA SEKTA YA KILIMO NCHINI

IMG_1670
Waziri wa Fedha na Uchumi Mhe Dk. Wiliam Mgimwa
Na Frank Mvungi na Eleuteri Mangi-MAELEZO
SERIKALI ya Tanzania imetiliana saini mkataba na Jumuiya ya  Umoja wa nchi za Ulaya( EU) utakaowezesha Tanzania kupatiwa shilingi bilioni 20 kusaidia maendeleo katika sekta ya kilimo cha miwa kwa wakulima wa Visiwa vya Zanzibar.
 Mkataba huo ulisainiwa jana jijini Dar es salaam kati ya Waziri wa Fedha na Uchumi Mhe Dk. Wiliam Mgimwa na Balozi wa EU Mhe. Filiberto Sebregondi, ambapo unategemewa kuisaidia serikali katika kuondoa umasikini kwa wananchi wake na kuiwezesha nchi kupiga hatua ya maendeleo kupitia sekta ya kilimo.
 Waziri Mgimwa alisema kuwa msaada huo pia utasaidia kuwajengea wananchi uwezo  wa kutekeleza kilimo chenye tija na kupanua soko la bidhaa zitokanazo na miwa kwani miundo mbinu ya maeneo ya Uzalishaji pia itaboreshwa katika utekelezaji wa mradi huo.
 “Kwa niaba ya Serikali  ya Jamuhuri ya Muungano wa Tanzania napenda kuishukuru jumuiya ya  umoja wa nchi za Ulaya kwa juhudi kubwa wanazochukua kusaidia maendeleo ya nchi yetu, asanteni sana,” alisema Waziri Dk.Mgimwa.
 Naye balozi wa EU, Mhe. Filberto Sebrigondi alisema wameridhishwa na mikakati ya serikali katika kuwaletea wananchi wake maendeleo ndio maana wanaendelea kuunga mkono juhudi za serikali ili kusaidia wananchi kufikia maendeleo ya kweli hivyo  wameamua kusaidia sekta ya miwa ili iweze kukua na kuchangia katika maendeleo ya Taifa.
 Pia balozi Sebrigondi alisema kuwa wataendelea kusaidia bajeti ya Serikali ya Tanzania katika miradi mbalimbali ya maendeleo kwa kuwa Tanzania imeonyesha nia ya dhati katika kukuza uchumi wake na kuweka mazingira mazuri kwa wananchi wake ili waongeze tija katika uzalishaji.
 Alisema katika kipindi kilichopita asilimia 87% ya fedha lizizotolewa kwa Serikali ya Tanzania zimeshatumika katika miradi ya maendeleo, hivyo ameahidi  kuwasaidia wanachi wanaojihusisha na kilimo cha miwa ili kuwajengea uwezo, kufanya tafiti na kutoa elimu ya utunzaji mazingira katika maeneo yatakayonufaika na msaada huo.
 Umoja wa nchi za Jumuiya ya Ulaya umekuwa kwa muda mrefu ukisaidia sekta mbalimbali za maendeleo hapa nchini ikiwa ni moja ya washirika wa maendeleo  wa Tanzania ambapo baadhi ya Sekta zinazonufaika ni sekta ya kilimo cha Kahawa, na Miwa, sekta ya Barabara, Elimu, nishati ya Umeme ambazo zimesaidia kwa kiasi kikubwa kukuza uchumi wa Tanzania.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.