Flaviana Matata atoa wito kwa serikali kuhusu ajali ya MV Bukoba

MARIAMiss Universe Flaviana Matata akiwa na Mkurugenzi wa Compass communicayion, Maria Sarungi wakiwasha mshumaa kwenye kaburi la Marehemu mama yake mzazi aliyefariki katika ajali ya MV Bukoba mwaka 1996.
……………………………………..
Na Mwandishi Wetu
MWANAMITINDO wa kimataifa wa Tanzania, Flaviana Matata ameiomba serikali kutangaza Mei 21 ya kila mwaka kuwa siku maalum ya maombolezo ya wasiku maalum ya maombolezo  ya wahanga wa MV Bukoba.
Ajali ya MV Bukoba ilitokea Mei 21 mwaka 1996 na kuua watu zaidi ya 1,000 na serikali kutangaza siku tatu za maombolezo ya kutokana na kuzama kwa meli hiyo iliyotokea kwenye  Ziwa Victoria. Katika ajali hiyo, Flaviana alipoteza mama na kaka yake.
Flaviana ambaye kwa sasa anafanya shughuli za kuonyesha mitindo nchini Marekani na Uingereza, amekuwa mstari wa mbele kuadhimisha siku hiyo kwa kupitia taasisi yake ya Flaviana Matata Foundation.
Akizungumza Kwa niaba ya Flaviana Matata Mkurugenzi wa Compass Communications Company Limited Maria Sarungi Tsehai alisema pamoja na ajali hiyo kuua watu wengi, lakini inasikitisha kuona jambo hilo kwa sasa limekuwa kama kumbukumbu kwa wahanga wa ajali hiyo tu na si vinginevyo.
Maria ambaye alisema hayo katika misa maalum ya kumbukumbu ya ajali hiyo iliyofanyika kwenye makabuli ya Igoma, Mwanza alisema kuwa wakati umefika sasa wa kutangaza siku ya kitaifa ya maombolezo na kwani ajali hiyo imeacha Watanzania wakiwa na huzuni kubwa.
Alisema kuwa wanashukuru sana kwa miaka hii miwili wamepata ushirikiano mzuri kutoka kwa Marine Service Company Limited na kampuni ya ndege ya Fastjet, ambapo mwaka jana walikabidhi vifaa vya kujiokolea (maboya) 500.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*