HII NDIO AJALI MBAYA YA BASI LA TAQWA ILIYOUA WATU NA MAJERUHI 44 IRINGA






Hili ndilo basi la Taqwa baada ya kupata ajali mbaya

Hii ndio ajali mbaya iliyoua 7 Iringa

Mwanahabari wa Nipashe Iringa Godfrey Mushi akimhoji mmoja kati ya majeruhi
Majeruhi wa ajali hiyo mbaya


WATU saba wamekufa papo hapo na wengine 44 kujeruhiwa vibaya baada ya basi la Kampuni ya Taqwa lililokuwa likitokea Jijini Dar es Salaam kwenda nchini Zimbabwe, kugongana uso kwa uso na lori la mizigo jana jioni katika Kijiji cha Nyololo,Wilaya ya Mufindi mkoani Iringa.

Ajali hiyo imeyahusisha magari matatu ambayo ni basi la Taqwa aina ya Nissan Disel lenye namba za usajili T 273 CBR (Sniper), lori la mizigo aina ya Scania, mali ya Kampuni ya Nyati Transport Ltd lililokuwa limebeba shehena ya viazi pamoja na lori la mizigo lenye namba T 104 BZZ aina ya Scania, mali ya kampuni ya Sogea Satom.

Kwa mujibu wa shuhuda wa ajali hiyo,Tsiesi Chipfupa ambaye ni raia wa Zimbabwe, ajali hiyo ilitokea majira ya saa 11 jioni ya Mei 3 mwaka huu baada ya lori la mizigo la Sogea Satom kutaka kulipita basi hilo kwa kasi na kusababisha basi la Taqwa kugongana uso kwa uso na lori la kampuni ya Nyati Transport na kusababisha vifo vya watu hao.

"Sisi tulikuwa tunatoka Dar es Salaam kwenda Harare (Zimbabwe) na tulipofika karibu na eneo la tukio, lori la mizigo (Sogea Satom) lilikuwa likitaka kutupita na ghafla nilisikia kishindo kikubwa na gari zima lilizizima kwa vilio. Nilijikuta nalia halafu wenzangu wanavuja damu nyingi lakini pia basi letu lilikuwa limefumuka lote sehemu ya mbele hadi katikati ambako huwezi kujua ni nini kimetokea kwa muda mfupi,"Alisema raia huyo wa Zimbabwe.

Ajali hiyo mbaya iliyotokana na mwendo kasi imetokea katika Kijiji cha Nyololo, kilomita 25 kutoka mji wa Mafinga.

Hadi jana mchana, bado waokoaji na maofisa wa Polisi wa usalama barabarani mkoa wa Iringa walikuwa wakihaha kuokoa mali za abiria hao, waliokuwa wakisafiri kutoka Dar es Salaam kuelekea nchi za Zimbabwe,Uganda na Malawi.

Akizungumza kwa tabu akiwa wodini katika Hospitali ya Mafinga,majeruhi wa jali hiyo, Rehema Gaifaro mkazi wa Mbeya aliyevunjika mguu wa kushoto na mkono wa kushoto ,alisema kuwa baada ya kutokea kwa ajali hiyo, dereva wa lori lililosababisha ajali ambalo ni mali ya kampuni ya Sogea Satom alikimbilia kusikojulikana.

"Nimevunjika mguu wa kushoto na mkono wa kushoto lakini mume wangu (Gaifaro Kaziulaya) ameumia mguu wa kushoto na mtoto wangu wa kike (Asnati Limma) yeye amejeruhiwa sehemu za mwili wake.Namshukuru Mungu kwa kutuepusha na kifo ingawa abiria wenzetu wametangulia mbele ya haki,"Alisema Rehema.

Hata hivyo, Mganga Mkuu wa Wilaya ya Mufindi, Dk.Erick Bakuza aliuambia mtandao huu wa www.matukiodaima.com kuwa hadi kufikia saa 1:00 jioni ya Mei 3 alikuwa amepokea miili saba ya marehemu na majeruhi 44 ambao wawili kati yao wapo mahututi kutokana na kuumia vibaya kichwani.

Alisema hadi jana,majeruhi watatu kati ya 44 walikuwa wameruhusiwa kuondoka hospitalini baada ya vipimo kubaini kuwa hawakupata majeraha makubwa yanayoweza kuwafanya waendelee kubaki wodini.

"Nimepokea majeuhi 44 na maiti saba wa ajali ya basi la Taqwa ambao walikuwa wakisafiri kuelekea nchi za Zimbabwe,Uganda na Malawi.Hali zao zinaendelea vizuri isipokuwa watu wawili ambao wako mahututi na wamelazwa chumba cha uangalizi maalumu (ICU) katika Hospitali hii ya Wilaya ya Mufindi (Mafinga)...Lakini changamoto kubwa hapa tunayoipata ni hapa ni namna ya kuwahudumia majeruhi wa ajali zinazotokea umbali wa kilomita 200 katika barabara kuu ya Iringa-Mbeya,"alisema Dk.Bakuza.

Dk.Bakuza aliwataja waliokufa kuwa ni Abrahaman Abduli (32) ambaye ni dereva wa basi la Taqwa,Nassoro Rashid (27) ambaye ni kondakta wa basi hilo,Omari Muhusin,Alli Mussa,Joseph Charles,Emmi Kafute na maiti moja haijafahamika jina lake.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA