KINANA AKAGUA HALI YA USALAMA NA AMANI ZIWA NYASA NA KUMUONYA RAIS BANDA

 Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (mbele) akiwa na Mwenyekiti wa CCM Mkoa wa Njombe, Deo Sanga, wakikagua hali ya usalama na amani katika mwambao wa Ziwa Nyasa eneo la Lupingu wakati wa ziara ya kiakazi ya siku saba ya kuimarisha uhai wa chama hicho mkoani Njombe leo. PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA
  Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana (wa pili kulia) akiwa na Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye (mbele) wakikagua hali ya usalama na amani katika mwambao wa Ziwa Nyasa eneo la Lupingu wakati wa ziara ya kiakazi ya siku saba ya kuimarisha uhai wa chama hicho mkoani Njombe leo. Kushoto ni Mbunge wa Jimbo la Ludewa, Deo Filikunjombe na Mbunge wa Mwibara, Kange Lugora.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA
 Katibu wa Itikadi na Uenezi wa CCM, Nape Nnauye akimsadia Agnes Haule kutwanga mhogo alipomkuta akitwanga katika Kijiji cha Lupingu, Ludewa leo.
 Kikundi la ngoma ya mganda kikitumbuiza  wakati wa mkutano wa hadhara uliohutubiwa na Katibu Mkuu wa CCM, Abdulrahman Kinana katika Kijiji cha Lupingu, mwambao wa Ziwa Nyasa, Ludewa.
 Mbunge wa Mwibara, mkoani Mara, Kange Lugora akiungana na Consolata Kayombo kucheza noma ya Chioda wakati wa mkutano huo.
 Wananchi wa Lupingu, mwambao wa Ziwa Nyasa wakimbeba Mbunge wa Jimbo hilo, Deo Filikunjmbe wakati wa mkutano huo.
 Wananchi wakila kiapo cha utii cha CCM wakati wa mkutano huo
Katibu Mkuu wa CCM, AKinana akijadiliana jambo na Mbunge wa Lu, Deo Filikunjombe baada ya kumaiziza kuhutubia mkutano wa hadhara

 KATIBU Mkuu wa Chama Cha Mapinduzi (CCM), Kanali Mstaafu Abdulrahman
Kinana, amemtumia salamu na kumuonya Rais wa Malawi Joyce Banda kwa kumwambia kuwa
Tanzania haitishwi na haiko tayari kuingia katika vita ya kugombania
mpaka wa Ziwa Nyasa.


Hata hivyo amesema kuwa Watanzania wana mambo mengi ya msingi ya
kuyashughulikia ikiwemo kusambaza huduma za maendeleo vijijini na sio
kuingia vitani kama anavyotaka rais huyo wa Malawi.
Akihutumia mamia ya wananchi wa Kata za Lupingu wilayani Ludewa mara
baada ya kutembelea mwambao wa Ziwa Nyasa na kujionea shughuli za
kiuchumi, alisema kuwa hatua ya vitisho vinavyotolewa hivi sasa havina
nafasi badala yake Tanzania inaamini katika majadiliano zaidi kuliko
kuingia vitani.
Katibu Mkuu huyo wa CCM, alisema kuwa pamoja na kulitumikia jeshi la
Wananchi Tanzania (JWTZ), kwa nafasi ya Kanali anajua kila aina ya
hadaha na mapambano lakini si kwenye kuingia vitani.
“Ni wazi nimetembelea ukanda huu wa mwambao wa Ziwa Nyasa na hata
kujionea namna mnavyofanya shughuli zetu za kiuchumi, lakini kutokana
na vitisho vinavyofanywa na yule mama wa Malawi ya kutaka watu
kutoelewana si sahihi hata kidogo.
“Pamoja na kusambazwa kwa ujumbe mbalimbali wa vitisho dhidi yenu hali
inayowafanya muishi kwa mashaka, ninachitaka kuwahakikishia laleni na
mfanye shughuli zenu bila tatizo na kubwa serikali yenu imejipanga kwa
kila hali.
“Suala la vita ni maneno ya kitoto ila kinachotakiwa kwenu kama taifa
ni kuweza kutumia fedha zetu kwa ajili ya shughuli za maendeleo kwa
watu wetu na si vinginevyo kama huyo mama anavyotaka.

Awali Mkuu wa Mkoa wa Njombe Kapteni mstaafu Assery Msangi, alisema
kuwa vyombo vya ulinzi na usalama vimekuwa vikifanya doria usiku na
mchana katika ukanda wote wa ziwa hasa upande wa Tanzania.
“Ninapenda kuwahakikishieni wananchi wote mnaoishi katika ukanda wa
Ziwa Nyasa fanyeni shughuli zetu kwa raha mustarehe, kwani tangu
vilipoanza vitisho na hata ujumbe  wa simu katika maeneo mbalimbali
serikali yenu imejipanga.
“Moja kati ya mambo yanayofanyika ni doria inayofanywa usiku na mchana
na vyombo vyetu vya ulinzi na usalama. Ninapenda kuwaonya wale ambao
wamekuwa na tabia ya kueneza ujumbe mfupi wa simu ambao una vitisho
waache mara moja.
“Tanzania haina nia hata kidogo ya kuingia katika mapambano na ugomvi
wa kivita na nchi jirani ya Malawi kwani tunajua wazi kuna ndugu zetu
wapo upande wa pili na hata wengine huvuka ziwa na kwenda kufanya
shughuli zao upande ule.
“CCM ni chama ambacho kimekuwa mstari wa mbele katika kupigania uhuru
wa nchi zilizo kusini mwa Afrika ili ziweze kujikomboa kutoka katika
makucha ya waloni na kufanya vinginevyo kwa Taifa letu tutakuwa ni
watu wa ajabu,” alisema Kapteni mstaafu Msangi.

Mwisho

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI