KUFUATIA MGOMO WA DALADALA IRINGA , SUMATRA YAKUNJUA MAKUCHA SASA YATISHIA KUWATIMUA KAZI MAOFISA WAKE .......
Mmiliki wa daladala akiwasilisha kero yake kwa uongozi wa Sumatra
Mmoja kati ya madereva hao na mmiliki wa daladala Bw Peter akitoa maoni yake kwa Sumatra.
Baadhi ya madereva wakitoa maoni yao juu ya kero wanazozipata
SAKATA
la mgomo wa daladala katika Manispaa ya Iringa limeanza
kushughulikiwa kwa kasi kubwa na mamlaka ya uthibiti ,usafiri wa majini
na nchi kavu (SUMATRA) makao makuu baada ya kutuma maofisa wake
kutoa elimu kwa wamiliki huku mamlaka hiyo ikiapa kuendelea kupambana
madereva wanaonyanyasa abiria kwa kuvunja wa sharia.
Pia
imeapa kuwachukulia hatua kali ikiwa ni pamoja na kuwafukuza kazi
maofisa wake ambao watabainika kupokea faini ndogo kinyume na faini
inayopaswa kulipwa kisheria.
Akizungumza
na wamiliki wa daladala na madereva leo katika ukumbi wa shule ya
Sekondari Lugalo , kaimu mkurugenzi wa idara ya usafiri wa barabarani
Bw Leo Ngowi alisema kuwa ni vema wamiliki wa daladala na madereva
kuheshimu sharia za usafirishaji ikiwa ni pamoja na kuzitambua sharia
hizo pia wasiwe nyume kuwafichua maofisa wanaukula rushwa .
Ngowi
alisema kimsingi katika sharia za Sumatra kuna faini za aina
mbili ikiwemo ya Tsh 500,000 ambapo nusu yake Tsh 250,000 na faini
nyingine ni Tsh 100,000 na nusu yake ni Tsh 50,000 na kuwa hakuna faini
ya chini ya hapo na iwapo kuna mtendaji anapokea chini ya viwango
hivyo atafukuzwa kazi mara moja.
Pia
Alisema kuwa mamlaka inapiga marufuku kwa madereva wa vyombo vya
usafiri kupakia wanyama kama mbuzi ,ama mkaa pamoja na vitu vingine
vya hatari kwa abiria .
Pamoja
na kuapa kuendelea kusimamia sharia bado SUMATRA afisa huyo
alisema kuwa utendaji kazi wake ni masaa 24 hivyo madereva
wasifikiri kuwa mamlaka hiyo ina muda wa maalum wa kufanya kazi .
Alisema
kuwa sheria hizo zimewekwa ili kuhakikisha kuwa sekta hiyo ya
usafiri inaboreshwa na kusiwepo kwa malalamiko kutoka pande mbili ya
mtoa huduma na mpokeaji wa huduma husika.
"
Sheria zinzohusu sekta ya usafirishaji ni pamoja na sharia ya
viwango ya mwaka 1975,sheria namba 30 ya mwaka 1973 ya usalama
barabarani sharia namba 1 ya 1973 ya leseni za usafirishaji na
sharia nyingine nyigi ambazo wanapaswa kuzitambua"
Hata
hivyo alisema kuwa kwa mujibu wa sharia za Sumatra haziruhusu
kwa daladala moja ama chombo kimoja cha usafiri kumiliki leseni
mbili za njia na kuwa iwapo wapo wanaofanya hivyo ni kinyume.
Ngowi
alisema kuwa kitendo cha daladala kushusha abiria njiani hata kama
ni abiria mmoja ni kosa na kuwa lengo la usafiri wa daladala ni
kushusha na kupakia na kuwa kwa kawaida usafiri wa mijini huwa haukai
sehemu moja kama ilivyo mabasi ya vijijini ambayo yamekuwa yakiegesha
sehemu moja kugonja abiria.
"Hakuna
sharia inayoruhusu usafiri wa mjini kukaa sehemu moja kwa zaidi ya
dakika 20 na kuwa kwa kawaida usafiri wa mjini ni kushusha na
kupakia na kuendelea na safari ...,kama kituo kimoja hakina abiria
basi kituo kinachofuata kitakuwa na abiria na hata kama kuna abiria
wawili ama mmoja haki yake ya msingi kufikishwa hadi mwisho wa safari
kwa mujibu wa leseni ya njia"
Aidha
alisema kuwa Sumatra imesitisha utoaji wa leseni kwa magari yenye
uwezo wa kubeba abiria kuanzia 7 hadi 12 iwapo yatatumika kwa
matumizi binafsi na namba za usajili ni zile za njano si vinginevyo .
Ngowi
alisema kuwa upande wa madereva ni lazima kabla ya kuanza kazi
kumfahamu vema mmiliki wa gari analoliendesha ikiwa ni pamoja na anuani
na namba za simu .
Pia
aliwataka madereva kukataa kuendesha gari iwapo litabainika kuwa ni
linaloweza kuhatarisha usalama wake na abiria wake .
Hata
hivyo alisema kuwa ni wajibu kwa mmiliki wa gari kumtafutia abiria
wake chakula iwapo gari hilo litaharibika kwa zaidi ya masaa mawili
na kuendelea ama sehemu ya kulala iwapo gari hilo halitaendelea na
safari na sharia hiyo kwa magari yanayofanya safari ndefu kwa maana
ya mikoa.
Wakati
kwa upande wa daladala ni marufuku kusimama kituoni kwa zaidi ya
dakika 5 katika kituo kimoja na kufanya hivyo ni kosa kisheria.
Kwa
upande wake mkurugenzi mtendaji wa Halmashauri ya Manispaa ya Iringa
Terresia Mahongo alisema kuwa lazima Sumatra kuweka mkakati wa
kuwasaidia wananchi ambao wameendelea kupata kero kubwa ya usafiri
kwa madereva wa daladala kuwakalisha abiria kwa muda mwingi eneo la
posta .
Kuhusu
suala la kukosekana kwa choo katika eneo la Isakalilo alisema kuwa
anawahakikishia madereva hao kuwa lazima kero hiyo ataifanyia kazi
ikiwa ni pamoja na kujenga choo mapema zaidi eneo hilo .
Wakati
madereva hao walilalamikia suala la ubovu wa barabara kuwa
baadhi ya njia kama ya Mikimbizi daladala zimekuwa zikikwepa kwenda
huko kutokana na njia hiyo kuwa na mawe mengi na njia kuwa mbovu kupita
kiasi hivyo wanataka suala la njia kurekebishwa zaidi.
Huku
mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa akiahidi kutengeneza barabara hizo
ndani ya wiki mbili zijazo ili kuwa na barabara nzuri zaidi.
Wakati
huo huo mkurugenzi wa Manispaa ya Iringa Bi.Mahongo amekataa ombi la
madereva na wamiliki wa daladala mjini Iringa la kutaka kikao kijacho
kati ya wadau wa usafiri na madereva na Manispaa kukutana majira ya saa 2
usiku na kuwa kwa muda huo hawapo tayari kufanya hivyo.
"
Mnataka tukutane usiku ili iweje pia na mimi ni kiongozi wa umma
ninalindwa na sharia za utumishi wa umma sasa mkisema tukutane usiku
sitakuwa tayari labdala iwe saa 10 jioni kama ambavyo baadhi yenu
mmependekeza iwe saa 10 jioni siku ya jumapili nipo tayari "
Hivyo
alisema kikao hicho kitakuwa cha wamiliki pekee wa daladala na si
vinginevyo huku akidai kuwa lazima chama cha madereva wa daladala mjini
Iringa kuchunguzwa upya kwani ndicho chanzo cha yote haya.
|
Comments