LEJENDARI DAVID BECKHAM: AAGA KWA USHINDI NA MACHOZI JUU PARIS!

Na Baraka Mpenja wa msaada wa Sportsmail.com, Soka In Bongo
DAVID BECKHAM alitoka Uwanjani katika Mechi yake ya mwisho ya Nyumbani ya Klabu yake Paris St-Germain ambayo huenda ikawa ndio ya mwisho katika maisha yake ya Soka ya Miaka 20 huku akibubujikwa machozi.
Beckham, ambae alianza Mechi hiyo ya Ligi dhidi ya Brest kama Nahodha, alibadilishwa katika Dakika ya 81 na Mechi kusimama kwa muda huku Wachezaji wenzake wa PSG wakimshangilia na yeye akawa akitoka nje kwa machozi.
Mashabiki wengi wa PSG wamekuwa wakililia Beckham, Miaka 38, abakie kama Mchezaji badala ya kustaafu.
Msimu huu PSG ndio wamekuwa Mabingwa wa France na bado wana Mechi moja ya Ligi  Jumapili ijayo watakayocheza Ugenini na Lorient lakini inaaminika Beckham hatakuwepo.
Katika Mechi ya Jana PSG waliifunga Brest Bao 3-1 huku Beckham akitengeneza Bao moja kwa Kona yake kuunganishwa na Blaise Matuidi na Bao nyingine mbili kufungwa na Zlatan Ibrahimovic.
Bao la Brest lilifungwa na Charlison Benschop.
Mara baada ya Filimbi ya mwisho kwenye Mechi hiyo na Brest, Beckham aliwahutubia Mashabiki na kusema: “Nataka kumshukuru kila Mtu hapa Paris-Wachezaji wenzangu, Wafanyakazi na Mashabiki. Ni kitu kikubwa kumalizia Soka langu hapa. Nimemaliza Soka nikiwa Bingwa na kwenye Timu iliyonifanya nijione kama nimekaa Miaka 10!”
Wachezaji wa PSG walimbeba na kumrusharusha juu huku akishuhudia na Mkewe Victoria na Rais wa zamani wa Ufaransa, Nicolas Sarkozy.
Proud: David Beckham was joined by his three sons with the Ligue 1 trophy after helping PSG to victory SIFA KUBWA: David Beckham aliungana na watoto wake kushangilia ubingwa ligi ya Ufaransa ambapo amewasaidia PSG kutwaa ndoo hiyo.
Up you go: After the final whistle, Beckham was flung into the air by his team-mates Baada ya kipenga cha mwisho, wachezaji wa PSG walikuwa wanamrusha Beckham juu
Upset: David Beckham applauded the fans as he left the pitch in tears after being substituted Baada ya kutolewa uwanjani hapo jana, Beckham alionekana akiwa hivyo
Moving: Beckham put the English flag around his neck for a lap of honour after the match
Teary: David Beckham burst into tears when he realised he was to be substituted by Carlo Ancelotti MACHOZI YAKIMTOKA: David Beckham alitokwa na machozi baada ya kuona kocha wake Carlo Ancelotti anataka kumtoa uwanjani ili kumpisha mchezaji mwingine
Teary: David Beckham burst into tears when he realised he was to be substituted by Carlo Ancelotti
One last time: David Beckham played his final ever game against Brest for PSG on Saturday evening MCHEZO WA MWISHO: David Beckham alicheza mexhi yake ya mwisho akiwa na PSG dhidi ya Brest hapo janaMoving: The PSG players hugged Beckham as he was substituted
Wachezaji wa PSG wakimkumbatia  Beckham baada ya kufanyiwa mabadiliko
Moving: The PSG players hugged Beckham as he was substituted

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.