MAKAMU WA RAIS DKT. BILAL ASHIRIKI MAADHIMISHO YA SIKU YA KIMATAIFA YA UTOKOMEZAJI WA UGONJWA WA FISTULA, JIJINI DAR

 3Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akizungumza na baba wa mtoto, Elizabeth Nora kutoka Dodoma aliyelazwa katika Hospitali ya CCBRT, wakati Makamu alipofika hospitalini hapo leo Mei 23, 2013 kwa ajili ya kushiriki katika  Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula. Picha na OMR 4Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisikiliza maelezo kutoka kwa Dokta wa Hospitali ya CCBRT, wakati alipokuwa akitembelea katika wodi za wagonjwa waliolazwa katika Hospitali hiyo, alipofika hospitalini hapo leo Mei 23, 2013 kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula. Kulia ni Mtoto Boniface Patrick akiwa na Baba yake, Patrick Luwao, Wakazi wa Dodoma, akiwa amelazwa baada ya kufanyiwa upasuaji na kuongezewa sehemu ya mguu uliokuwa mfupi. Picha na OMR 5Makamu wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania, Dkt. Mohammed Gharib Bilal, akisalimiana na Stellah Nzyemba, ambaye awali alikuwa mgonjwa na baada ya kutibiwa katika Hospitali hiyo ya CCBRT na kupona ameajiriwa ili kuwasaidia wagonjwa wa Fistula. Makamu alifika hospitalini hapo leo Mei 23, 2013 kwa ajili ya kushiriki katika Maadhimisho ya Siku ya Kimataifa ya Utokomezaji wa Ugonjwa wa Fistula. Picha na OMR 8Makamu wa Rais Dkt Bilal, akimjulia hali mtoto mgonjwa aliyelazwa katika Hospitali hiyo ya CCBRT. 10Makamu wa Rais Dkt. Bilal, akiwasili katika eneo lililoandaliwa maalum kwa ajili ya kufanyia shughuli za maadhimisho hayo. 11Balozi wa Uingereza nchini, Dianna Melrose, akizungumza wakati wa maadhimisho hayo. 12Balozi wa Ugonjwa wa Fistula, Msanii wa Muziki wa Kizazi kipya, Mwana FA, akisoma hotuba yake kuhusiana na kuzunguka katika baadhi ya mikoa na kutoa ujumbe kwa wananchi na hasa kina mama kuhusu Ugonjwa huo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.