MBUNGE LUKUVI AMPONGEZA RAIS KIKWETE KWA UJENZI WA BARABARA YA IRINGA- DODOMA- live

Rais  Kikwete  akisalimiana na mwenyekiti wa CCM wilaya ya  Kilolo Sety Moto leo
Wakurugenzi  wa Halmashauri ya Manispaa ya  Iringa na Iringa  vijijini wakiwa katika  uwekaji  wa  jiwe la msingi barabara ya Iringa - Dodoma  leo eneo la Migoli Mtera
Rais Jakaya  Kikwete (kushoto) akiteta  jambo na mbunge wa  jimbo la Isimani Wiliam Lukuvi  leo

 watumishi  wa mahakama kuu kanda ya  Iringa  pia wamepata  kushiriki
.............................................................................. 

MBUNGE  wa  jimbo la Isimani wilayani  Iringa mkoani Iringa  Bw. Wiliam Lukuvi amempongeza  Rais Jakaya  Kikwete  kwa  kuwawezesha  wakazi  wa tarafa  ya Isimani kuweza  kuanza  kushuhudia mapinduzi makubwa ya  kimaendeleo kupitia mradi mkubwa  wa barabara  ya  kiwango  cha lami kutoka Iringa - Dodoma  inayopita katika   tarafa  hiyo .
 
Lukuvi  ambae ni  waziri  wa nchi  ofisi  ya  waziri  mkuu (sera na uratibu  wa  bunge) alisema  kuwa  barabara  hiyo ambayo ni ukombozi mkubwa kwa nchi  za  kusini mwa  Tanzania  ilikuwemo katika mkakati  wa kujengwa kwa kiwango  cha lami kwa kitambo  kirefu na  kila awamu  wananchi  walikuwa  wakiulizana  juu ya kuanza  kwa mradi huo.
 
Hata  hivyo  alisema  baada ya awamu  hii ya nne  chini ya  Rais Kikwete  wananchi hao  wameweza kushuhudia  majibu ya maswali yao  kwa  kuanza  kwa ujenzi huo ambao  kila mmoja anatambua  kama ni ukombozi katika  sekta ya maendeleo.
 
Waziri  Lukuvi alitoa  pongezi  hizo kwa Rais Kikwete  leo wakati akiwasalimia  wananchi  wa  jimbo  la Isimani ambao  walishiriki hafla  fupi ya Rais Kikwete  kuweka jiwe 
 
Kwa  upande  wake  Rais Jakaya  Kikwete  alisema  kuwa  mbali ya  serikali  kujipanga kwa  ujenzi  wa barabara bado lengo la  serikali ni  kuhakikisha nchi  nzima inaunganishwa kwa mtandao  wa barabara  ya lami na kuwa kazi hiyo tayari  imeanza.
 
Alisema  kuwa serikali  yake  toka  imeingia madarakani  imeendelea  kuongeza  fedha  katika mfuko  wa barabara  na kuwa lengo ni kuendelea  kuongeza  zaidi fedha katika mfuko  huo ili  kuwezesha  ujenzi  wa barabara nchini kuweza  kukamilika 
 
 Rais  Kikwete  pia amewapongeza  viongozi wa TANROADS kwa kazi nzuri  wanayoendelea  kuifanya na kwa  mbali ya kupongezwa bado hawapaswi kulewa  sifa na badala  yake  kuendeleza  jitihada za  kusimamia  kazi  hiyo kwani upo usemi unao sema kuwa mgema akisifiwa pombe huweka maji .
 
Pia  Rais Kikwete alimpompongeza  waziri wa fedha Dkt Wiliam Mgimwa kwa kuendelea  kuidhinisha  fedha kwa ajili ya miradi ya barabara hapa nchini na kuwa  bila  wizara  hiyo  kutenga bajeti  kazi hiyo ingeendelea  kuwa ngumu.






Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI