MSIMU WA TATU WA GUINESS FOOTBALL CHALLENGE: NUSU FAINALI

Dar es Salaam: Mei 22, 2013 Juma tano usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV tumeona nusu fainali ya kwanza ya GUINNESS® FOOTBALL CHALLEGE™ ambapo timu ya Ghana walionesha kuwa wao ni timu bora baada ya kushinda na kuwa timu iliyoshinda kiasi kikubwa zaidi cha pesa.


Jonathan Nabb na Desmond Odaano walionesha kuwa wana uwezo na ni majasiri walipowashinda wapinzani wao na mwisho kushinda kitita cha dola za kimarekani 12,000 baada ya kulenga kitundu namba nne katika hatua ya pesa ukutani.


Watakaorudi nyumbani ni Daniel Msekwa na Mwalimu Akida Hamad kutoka Dar-es-Salaam wakiwa na na dola 5,500 walizojipatia katika hatua za kitaifa. Sasa kazi itakuwa kwa timu mbili za Kenya katika nusu fainalli ijayo watakapokuwa wakiiwakilisha Afrika mashariki.


Washindi Jonathan na Desmond, walizawadiwa pia dola za kimarekani 4,000 baada ya kuonesha mchezo mzuri sana katika mizunguko miwili ya mwanzo ya mchezo ambapo hawakukosa hata swali moja. Sasa wamefanikiwa kuingia katika fainali ya Pan-african na kujihakikishia  na hata kuwa washindi wa mashindano hayo.


Kutoka Nairobi Kenya, Francis Ngigi na Kepha Kimani ambao wameshika nafasi ya pili wataungana pia na washindi wa kwanza Jonathan na Desmond katika hatua ya fainali. Japokuwa hawakufanikiwa kufikia hatua ya pesa ukutani lakini wamefuzu kuingia fainali. Wenzao kutoka Kenya Kenneth Kumau na Wills Ogutu hawakufanikiwa kufuzu hivyo Francis na Kepha ndio watakaoiwakilisha Afrika mashariki. 


Meneja wa kinywaji cha Guinness Davis Kambi alisema,”Sote Tanzania tunawapongeza Daniel na Mwalimu-japokuwa hawakufanikiwa kufuzu fainali lakini  wamejishindia kiasi kikubwa cha pesa. Kila timu ilijitahidi kufikia nusu fainali na hongera kwa Desmond na Jonathan kutoka Ghana kwa ushindi wao. Sasa tunasubiri nusu fainali ijayo kila la heri kwa wote pamoja na timu za Kenya zitakazowakilisha Afrika mashariki”


Watakaoingia uwanjani katiaka nusu fainali ya pili kuwania nafasi mbili za kucheza fainali:


AFRIKA MASHARIKI:

·         JEZI NYEUSI – Ephatus Nyambura(24) na Samuel Papa(23) kutoka Nairobi watatarajia kushinda zaidi ya dola 3,000 walizopata katika hatua za kitaifa na robo fainali. Ephatus atajibu maswali wakati Samuel anayechezea Nakuru Allstars atakuwa akionesha uwezo wa kusakata kabumbu.

·         JEZI NYEKUNDU – Kenneth Mukuri (26) na Chris Mwamgi (19) kutoka Nairobi watakuwa wakitarajia kushinda zaidi ya dola 1,500 walizopata katika hatua za kitaifa. Kenneth atakuwa kichwa cha timu wakati Chris atakuwa akionesha uwezo wake wa kisoka


CAMEROUN:

·         JEZI ZA KIJANI – Emerald Tchouta (24) na Abdul Sam (25) ambao wana jumla ya dola 6,500 baada ya kulenga lengo namba nne katika robbo fainali. Sasa Emerald na Abdul watacheza kuwania nafasi ya kufuzu fainali.


GHANA:

·         JEZI ZA BLU – Emanuel Kofi Okarku (27) na Isaac Aryee (25) kutoka Accra Ghana wataiwakilisha nchi yao kutoka Afrika magharibi ili kufuzu fainali. Tayari wana dola za kimarekani 3,000 hivyo Isaac atahitajika kuonesha kipaji chake cha kucheza  soka wakati Emanuel atajibu maswali.


Wapenzi wa kipindi hiki cha Guinness football challenge wanaweza kupima maarifa yao katika soka kupitia GUINNESS® VIP™.  Wanaweza kufanya hivyo kwa kujisajili bure kabisa katika m.guinnessvip.com kwa kupitia simu ya mkononi.  


Usikose kufuatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.

-www.facebook.com/guinnesstanzania


Nusu fainali ya pili ya mashindano haya imeandaliwa na kutengenezwa  na Kampuni ya kimataifa ya Endemol, na kurushwa na Televisheni ya ITV siku ya Jumatano saa 3:15 usiku, huku ukiburudika na bia yako ya Guinness.


Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.


Notes to Editors:

The GUINNESS and FOOTBALL CHALLENGE, and GUINNESS VIP words and associated logos are trade marks

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.