MZEE WA MIAKA 65 MKAZI WA MAJENGO KAHAMA, MBARONI KWA KUBAKA MTOTO WA MIAKA 6.

MKUU WA POLISI WILAYA YA KAHAMA GEORGE SIMBA.



KAHAMA
Jeshi la Polisi wilayani Kahama mkoani Shinyanga kwa kushirikiana na wananchi wamefanikiwa kumtia mbaroni mzee  wa mika 65 aliyembaka binti wa miaka sita anayesoma chekechea. 
Kwa mujibu wa mkuu wa Polisi wilayani Kahama George Simba ameiambia Blog hii  kuwa mtuhumiwa huyo alitenda kosa hilo May 19 mwaka huu saa 12 jioni eneo la Majengo wilayani Humo.
Akiendelea kufafanua Simba amemtaja mtuhumiwa kuwa ni Mageta Singu anayefahamika pia kwa jina la Babu kabila msukuma kazi ni mkulima ambaye ni mkazi wa Majengo wilayani Kahama.
Imeelezwa Baada ya kufanya kosa hilo mtuhumiwa alitokomea kusikojulika ambapo jeshi la Polisi kwa kushirikiana na Wananchi waliendelea na msako hadi kufanikiwa kumkamata leo asubuhi maeneo ya majengo wilayani humo.
Kwa mujibu wa Kamanda Simba amesema kuwa kwa sasa mtuhumiwa yupo chini ya ulinzi kwa mahojiano na jeshi la Polisi linaendelea na uchunguzi na pindi ukikamilika mtuhumiwa atafikishwa mahakamani kujibu shitaka la ubakaji.
Kutokana na matukio ya ubakaji kuwa mengi Wilayani Kahama,Jeshi la Polisi wilayani humo kupitia dawati la Jinsia limeweka mikakati thabiti ikiwa ni pamoja na kutoa elimu kwa mabinti  na wazazi kwa ujumla ili kujua na kuviepuka vyanzo hatarishi vya ubakaji.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.