NI TIMU KUTOKA AFRIKA MASHARIKI USO KWA USO NA AFRIKA MAGHARIBI FAINALI YA PAN-AFRICAN GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE

 Okraku Kofi & Isaac Aryee - Ghana
 Ephantus Nyambura & Samuel Papa - Kenya

Mei  29, 2013 Jana usiku kupitia televisheni za ITV na Clouds TV timu pinzani kutoka Afrika zilipambana vikali kufuzu nafasi mbili kuingia katika fainali ya Pan–African Guinness Football Challenge .

Timu yetu ya Kenya kutoka Afrika mashariki, Ephatus Nyambura na Samuel Papa walikusanya alama 14 katika mzunguko wa muundo na wakafikia hadi hatua ya penati baada ya kuishinda timu ya Cameroon.Wakiwa washindi wa pili wa mchezo bado wana nafasi ya kushinda katika fainali ya mashindano haya.Waghana Emmanuel Kofi Okarku na Isaac Aryee walifanikiwa kufikia hatua ya ukuta wa pesa wa Guinness.

Ephatus, Samuel pamoja na Emmanuel na Isaac sasa watakutana na Desmond, Jonathan, Francis Ngigi na Kepha Kimani kufanya timu nne katika fainali ya Pan-African. Hawa wote wana nafasi ya kupeperusha bendera ya nchi zao, lakini watahitaji kujiandaa vizuri na kuwa makini ili waweze kushinda taji la Pan-African Guinness Football Challenge.

Watakaokutana katika fainali ya mashindano ya Pan-African GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE  watakuwa ni timu mbili kutoka Afrika mashariki na mbili kutoka Afrika magharibi. Kutoka  Afrika mashariki ni Ephatus Nyambura, Samuel Papa, Francis Ngigi  na Kepha Kimani.
Ushindani kati ya Afrika Mashariki na Afrika Magharibi utakuwa mkali,ni upande upi wa bara  utakaoshinda taji hili?

Fainali ya mashindano ya GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE, yanayoandaliwa na Endemol , itarushwa na televisheni za ITV na Clouds TV siku ya Jumatano saa 3:15 usiku ITV na saa 2:15 usiku Clouds TV kwa hiyo hakikisha unaangalia mchezo huu huku ukiburudika na kinywaji cha GUINNESS.

Usikose kufuatilia ukurasa wa facebook wa GUINNESS FOOTBALL CHALLENGE kwa habari mbalimbali.
-www.facebook.com/guinnesstanzania


Tafadhali kunywa kistaarabu- Hairuhusiwi kuuzwa kwa wale wenye umri chini ya miaka 18.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI