RAIS KIKWETE AWATIA HAMASA TAIFA STARS

 Rais Jakaya Kikwete akipita katikati ya wachezaji wa Taifa Stars tayari kwa tukio la kupiga picha nao, Ikulu, Dar es Salaam.PICHA ZOTE NA KAMANDA RICHARD MWAIKENDA)
 Rais Jakaya Kikwete (mstari wa mbele katikati) akiwa na wachezaji wa timu ya soka ya Taifa (Taifa Stars), pamoja na wajumbe wa Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars Ikulu, Dar es Salaam leo, ambapo aliwaita kula nao chakula cha mchana na kuwapa hamasa ya ushindi dhidi ya Morocco na mechi zingine watakazokabiliana nazo katika michuano ya kuwania kufuzu Fainali za Kombe la Dunia 2014
 Wachezaji wakipata chakula cha mchana walichoandaliwa na Rais Kikwete, Ikulu, Dar es Salaam



 Rais Jakaya Kikwete akizungumza na wanakamati ya ushindi wa Taifa Stars, Waziri wa Habari, Vijana Utamaduni na Michezo, Dk. Fnella Mkangara pamoja na Kocha wa Taifa Stars, Kim Poulsen.
 Wachezaji wa Taifa Stars wakimsikiliza Rais Kikwete alipokuwa anazungumza nao baada ya chakula

 Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo akizungumza kabla ya kumkaribisha Rais
 Rais Jakaya Kikwete akiwapa hamasa wachezaji wa timu hiyo
 Nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja akiahidi mbele ya Rais Jakaya Kikwete kwamba watafanya juu chini kupata ushindi katika mechi zote zilizobakia.
 Rais Jakaya Kikwete (katikati) na Rais wa Shirikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga (kulia) pamoja na Kaimu Mwenyekiti wa Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars, Dk. Ramadhan Dau wakifurahi baada ya Nahodha wa Taifa Stars, Juma Kaseja kuahidi ushindi dhidi ya Morocco.
 Kocha Mkuu wa Tgaifa Stars, Kim Pousen akiahidi ushindi mbele ya Rais
 JK akiagana na Rais wa Shurikisho la Mpira wa Miguu Tanzania (TFF), Leodger Tenga
 JK akiagana na mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars, Teddy Mapunda
 JK akiagana na Mwenyekiti wa Baraza la Michezo Tanzania, Dioniz Malinzi
 JK akiagana na George Kavishe mjumbe wa Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars na Meneja wa bia aina ya Kilimanjaro wadhamini wakuu wa Taifa Stars.

 Rais akiagana na wachezaji wa Taifa Stars


Na Veronica Kazimoto –MAELEZO
 Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Jakaya Mrisho Kikwete leo amekutana na timu ya Taifa (Taifa stars) kwa lengo la kuitia moyo katika mechi ijayo kati yake na timu ya Moroco ikiwa ni harakati za Tanzania kutafuta tiketi ya kucheza fainali za kombe la Dunia kwa mara ya kwanza  mwaka 2014.
Rais Kikwete ameiambia timu hiyo kuwa ina uwezo mkubwa  wa kusonga mbele kutokana na uwezo mkubwa waliouonesha katika mchezo wao  dhidi ya Gambia ambapo walifanikiwa kupata  ushindi wa bao 2-0.
 “Maadamu mara ya kwanza mliwashinda Gambia, hakikisheni pia mnapata ushindi dhidi ya Moroco, mkishinda tunafurahi sana na mkishindwa tunanyong’onyea sana,” amesema Rais Kikwete.
 Aidha amempongeza kocha wa timu hiyo Kim Poulsen  pamoja na Kamati ya Taifa ya ushindi ya Taifa stars kwa kuisaidia timu hiyo kiasi cha shilingi milioni 30 ikiwa ni mkakati wa kuiongezea nguvu kwa hatua iliyofikia  na kuwataka wachezaji kujituma ili kuwafurahisha watanzania ambao hivi sasa wanaipenda timu yao ya Taifa.
 Nae Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Fenera Mukangara amesema Serikali itaendelea kushirikiana na wadau mbalimbali wa michezo nchini  ili kuondoa changamoto zinazoikabili timu hiyo.
 Kwa upande wake Kocha Poulsen, amemshukuru Rais Kikwete kwa kuwakaribisha na kuwatia moyo ambapo ameahidi kuifundisha vizuri timu hiyo ili kuhakikisha kuwa wanapata ushindi.
 Akizungumza kwa niaba ya wachezaji wenzake nahoidha wa timu hiyo Juma Kaseja amemshukuru Rais Kikwete na kuahidi kujituma kwenye mazoezi na hatimaye kuibuka washindi  kwenye mechi zijazo.
 Taifa stars ambayo inakamata nafasi ya pili katika kundi C inatarajia kucheza ugenini na Morocco mnamo Juni 7 mwaka huu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU