SHERIA YA KUSIMAMIA VYOMBO VYA HABARI KUWASILISHWA BUNGENI

Na Lydia Churi, MAELEZO-DODOMA                                      
Serikali imeridhia kutungwa kwa sheria ya Kusimamia vyombo vya Habari ambapo muswada wa kutunga sheria hiyo utawasilishwa bungeni hivi karibuni.
Akisoma hotuba ya bajeti ya Wizara yake bungeni mjini Dodoma leo, Waziri wa Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo Dkt. Fenella Mukangara alisema baada ya sheria hiyo kupitishwa na bunge, Wizara itaanza kuandaa waraka wa mapendekezo ya kutunga sheria ya Haki ya kupata Habari wakati serikali ikiendelea na utafiti ili kupata uzoefu kutoka nchi mbalimbali zenye sheria hii.
Kwa mujibu wa Dkt. Mukangara kutungwa kwa sheria ya kusimamima vyombo vya habari kutasaidia katika kuimarisha tasnia ya habari nchini na kupunguza kwa kiasi kikubwa changamoto zinazoikabili wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo likiwemo suala la mafunzo kwa waandishi wa habari  pamoja na mazingira duni ya kazi.
Katika hotuba yake Dkt. Mukangara alisema pia Wizara yake imeazimia kutekeleza suala la uanzishwaji wa benki ya Vijana ya Taifa katika mwaka wa fedha wa 2013/2014.
Aliongeza kuwa Wizara pia itaboresha huduma ya Mfuko wa Maendeleo ya mikopo yenye masharti nafuu kwa vijana pamoja na kuendelea kuzijengea uwezo SACCOS zinazotoa huduma kwa vijana.
Wizara ya Habari, Vijana, Utamaduni na Michezo inaomba kuidhinishiwa bajeti ya jumla ya shilingi 21,328,045,000 ambapo  kati ya fedha hizo, fedha za matumizi ya kawaida ni 20,728,045,000 na fedha za miradi ya maendeleo ni shilingi 600,000,000

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*