STREKA WA ATLTICO REAL RADAMEL FALCAO KWENDA MONACO UFARANSA KUPIMWA AFYA ILI KUKITUMIKIA KLABU HIYO MSIMU UJAO.

Chelsea Transfer News: Radamel Falcao Will Be A Chelsea Player In JanuarySTRAIKA HATARI wa Atletico Madrid, Radamel Falcao, atapimwa afya yake kwenye Klabu ya Monaco ambayo imepanda Daraja Msimu huu kurudi Ligue 1 ya France na Uhamisho wake unatarajiwa kugharimu Dau la Pauni Milioni 51.

Habari hizi zimevuja huko Spain na kudaiwa kuwa Atraika huyo kutoka Colombo atapimwa afya yake leo Jumatatu Mei 27. 

Monaco, ambayo imenunuliwa na Tajiri wa Kirusi Dmitry Rybolovlev, tayari imeshawanunua Mastaa wa FC Porto Joao Moutinho na James Rodr
iguez kwa Dau la Jumla ya Pauni Milioni 60 na kutua kwa Falcao kutawafanya watatu hao wakutane tena kwani waliwahi kuchezea Klabu moja.
Kuhama kwa Falcao kulidokezwa na Meneja wa Atletico Madrid Diego Simeone ambae ameshasema hatakuwa na kinyongo ikiwa Falcao, mwenye Miaka 27, atahama. 

Hivi Juzi, Kocha Msaidizi wa Monaco, Jean Petit, alidokeza wanatarajia Falcao na Wachezaji wengine wanne au watano wa kiwango chake kununuliwa na Klabu yao.
Mwezi Desemba 2011, Dmitry Rybolovlev alinunua Hisa za Asilimia 60 za Klabu ya Monaco na kuanza kuibadili wakati huo ikiogelea Daraja la chini huko France, Ligue 2, na Mwezi Mei 2012 alimteua Kocha wa zamani wa Chelsea Claudio Ranieri kuiongoza Monaco na amefanya hilo kwa mafanikio kwa kuirudisha Monaco Daraja la juu huko France.

STRAIKA HATARI wa Atletico Madrid, Radamel Falcao, atapimwa afya yake kwenye Klabu ya Monaco ambayo imepanda Daraja Msimu huu kurudi Ligue 1 ya France na Uhamisho wake unatarajiwa kugharimu Dau la Pauni Milioni 51

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI