Pichani
ni viongozi wa taifa letu mwanzoni kabisa mara tu baada ya kupata uhuru
mwaka 1961.Jambo moja ambalo limetuvutia mpaka kuamua kuweka kumbukumbu
hii ni mavazi ya “waheshimiwa”.Ukitizama utaona kwamba kumbe wakati
tunapata uhuru,wengi miongoni mwa viongozi wetu,walikuwa wanathamini
mavazi ambayo hata kwa kuyatizama tu unaweza kutambua kwamba ni mavazi
ya “kiafrika”.
Sasa
nini kilitokea baada ya hapo?Mbona leo hii ni nadra sana(kama huwa
inatokea) kuwaona viongozi wetu wakitukuza mila,tamaduni na desturi zetu
japo kuanzia kwenye mavazi tu?Mbona wenzetu wa sehemu zingine za Afrika
kama vile Afrika Magharibi wao wanaendelea kujinadi na mavazi yao ya
asili?Ni kweli kwamba sisi hatuna vazi la taifa au tumezembea tu kuwa
nalo?
Je unawatambua viongozi unaowaona pichani?Kama jibu ni ndio basi tusaidiane katika kuweka kumbukumbu sawa.Shukrani za pekee kwa Michuzi kwa kuhifadhi picha za kumbukumbu kama hizi.
Comments