Uhuru wa vyombo vya habari ni changamoto

Jakaya+Kikwete+Obama+Delivers+Address+Symposium+sfjZO4OTwTvl[1]

Na Claudia Kayombo wa Jambo Leo

LEO wanahabari wa Jumuia ya Afrika Mashariki, wanaungana na wenzao duniani kuadhimisha siku ya Uhuru wa Vyombo vya Habari.
Miongoni mwa mambo ambayo yanatarajiwa kutawala wakati wa maadhimisho hayo ya siku tatu, ni majadiliano ya namna ya kuondoa utata wa mazingira ya waandishi wa habari kufanyia kazi hususan nchini Tanzania.
Maadhimisho hayo kwa ukanda huo, yanaadhimishwa mkoani Arusha Tanzania.
Hata hivyo wakati katika Jumuia ya Afrika Mashariki wawakishi wakikutana Arusha, kwa upande wao waandishi wengine wanayaadhimisha kwa kila mkoa kupitia klabu zao.
Wakati maadhimisho hayo yakifanyika, vichwa vya wanahabari nchini, vimebeba wasiwasi baada ya miaka ya hivi karibuni kutokea matukio yanayotishia usalama wa maisha yao.
Mashaka katika vichwa vya waandishi yamekuja baada ya matukio mawili ya vifo vya waandishi na la tatu la kutekwa, kung’olewa jicho, meno kwa mmoja wa nguli wa tasnia hiyo, Absalom Kibanda.
Katika mazingira yanayoonesha kuwa, Kibanda pengine aliponzwa na ukali wa kalamu yake, ni pale aliposubiriwa katika geti la nyumba yake na kufanyiwa unyama huo.
Katika mikutano kadhaa niliyohudhuria ambayo inamzungumzia, Kibanda kila mwanahabari alionesha mashaka kuwa baada ya Kibanda anayefuata ni yeye iwapo vyombo vya ulinzi na usalama havitalivalia njuga jambo hilo.
Mkurugenzi Mtendaji wa Mfuko wa Vyombo vya Habari Tanzania (TMF), Ernest Sungura anasema mazingira ya mwandishi wa habari kufanya kazi na kuishi hapa yana utata mkubwa.
Sungura anasema licha ya kwamba miaka michache iliyopita kulikuwa na vitisho dhidi ya waandishi wa habari za uchunguzi lakini hawakuwa wakiguswa kwa maana ya kuathiriwa kwa kupigwa.
Anatolea mfano yeye mwenyewe kuwa bosi wake kwa wakati huo ambaye alikuwa na mazoea ya kuacha nywele ndefu alilazimika kubadili mtindo wa unyoaji baada ya kutafutwa na askari polisi mara kwa mara.
Ukweli wa mambo ni kwamba maadhimisho ya siku ya Uhuru wa Vyombo vya habari duniani yawe mwanzo wa kukoma kwa vitendo vya ukatili dhidi ya wanahabari nchini.
Pia iwe chachu kwa wamiliki wa vyombo vya habari kuwalipa waandishi wa habari mishara yao kwa wakati kwani hiyo ni changamoto ambayo sasa ipo katika ofisi nyingi za vyombo vya habari hivyo kuwafanya wageuke kuwa ombaomba au wasaliti wa fani hiyo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*