WANANCHI KUSAFIRI TOKA MTWARA HADI BUKOBA KWA LAMI
Na Immaculate Makilika- Dodoma
WANANCHI
wataweza kusafiri kutoka Mtwara hadi Bukoba kwenye barabara ya
lami,hayo yamesemwa mapema leo hapa Bungeni Mjini Dodoma wakati
Waziri wa Ujenzi John Magufuli alipokua akijibu swali la Martha
Mlata(Viti Maalum-CCM), swali lililohoji juu ya ahadi ya Serikali
katika kipindi cha awamu ya nne na ahadi hiyo iliyosema wananchi
wataweza kusafiri kwa taxi toka Mtwara hadi Bukoba,Je utekelezaji
wa ahadi hiyo umefikia wapi.Aidha Waziri Magufuli alisema kuwa nia ya
msemo huo ni kuonesha kwamba wananchi wataweza kusafiri toka Mtwara
hadi Bukoba kwa lami na kuongeza kuwa lengo hilo limetekelezwa kwa
mafaniko makubwa hadi kufikia asilimia 99 ya barabara yote kutokea
Mtwara hadi Bukoba.
Hata
hivyo Magufuli aliendelea kwa kwa kusema kwamba barabara yote kuanzia
Mtwara – Dar es Salaam- Dodoma-Singida- Nzega-Tinde-Usagara pamoja na
Geita-Bwanga-Kyamyorwa hadi Bukoba yenye urefu wa kilometa zipatazo
1,989 imejengwa kwa kiwango cha lami.
Isipokua
sehemu fupi yenye urefu wa takribani kilometa 26 katika barabara ya
Ndundu-Somanja ambayo itakamilika kujengwa kwa kiwang o cha lami kabla
ya Desemba,2013
Serikali ya awamu ya nne itahakikisha ahadi ya wananchi kusafiri kwenye barabara ya lami toka Mtwara hadi Bukoba inatekelezwa.
Comments