WASANII 320 KUJIMWAGA JUKWAANI KUONESHA VIPAJI SIKU YA TAMASHA LA MASTAA CHIPUKIZI!!

101_0267
Mwenyekiti wa Shiwata, Caasim Taalib (Kulia)
TAMASHA la Mastaa chipukizi zaidi ya 320 la mwezi Mei litafanyika Jumapili 26, 2013 katika ukumbi wa Starlight Hotel kuanzia saa 4 asubuhi mpaka saa 10 jioni.
 Mwenyekiti wa Shiwata, Caasim Taalib alisema maandalizi ya tamasha hilo yamekamilika  na vikundi vya sanaa vya Kaole, Splendid, Super Shine Taarab, Five Star Modern Taarab pamoja na wasanii mbalimbali wa Bongo Flava, Maigizo,Ngoma, Dansi na Sarakasi nao wamethibitisha kushiriki.
 Taalib alisema wasanii wakongwe wa bongo flava walioalikwa ni Stara Thomas, Ommy G na waigizaji wakongwe wa Kaole na Splendid wataonesha umahiri wao katika fani ya sanaa Kauli Mbiu ikiwa ni Kilio cha Msanii .
 Vikundi vingine vitakaonesha vipaji vyao ni Kepteni  Shaibu, Tanzania Disabled, Uyoga Boga Village, Ndafu Arts Group, CGC, Magengistar Crew, Dodo Arts Group, Culture Arts Group, Wachapa Kazi Academy, Soweto Picture, Shiwata Commedy, Mwavionelachi, Manuari Arts Group, Tandale Morden Taarab na Begeja Wushu,
 Wakati huo huo SHIWATA inawapongeza wote walioshiriki tamasha  la Aprili 27 ambako zaidi ya wasanii 300 walishiriki kuonesha vipaji.
 Pia Taalib amelipongeza Shirikisho la Filamu Tanzania (TAFF) kwa ushirikiano wao mzuri na kuwaomba viongozi wengine wa bendi za muziki, taarab,vikundi vya sanaa,mapromota,maprodusa na wadau wote kushiriki katika matamasha haya ili kujenga ushirikiano wa pamoja.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*