Wateja wa benki waanza kuelimishwa kunufaika na huduma ya M-pesa benki popote


Mteja wa wa Benki ya Amana Suleiman Mahmud akielezea namna anavyoifahamu huduma ya kutoa na kuweka fedha kwenye akaunti ya Benki hiyo kwa njia ya M-pesa wakati wa zoezi la kuelimisha wateja kuhusu huduma ya M-pesa  benki popote iliyofanyika katika Tawi la Kariakoo jijini Dar es salaam. Wanaomsikiliza ni Meneja wa Uhusiano wa Mambo ya Nje wa Vodacom Tanznaia Salum Mwalim (wa kwanza kulia), Meneja Masoko wa Benki ya Amana Fatma Mruma (wa Kwanza kushoto) na kaimu Meneja wa Tawi hilo Khamis Gumbo.

Kampuni ya Vodacom imeanza kuwapatia wateja wa benki za biashara ambazo zimeunganishwa na mtadao wa huduma za M-pesa elimu ya ufahamu wa namna ya kutumia huduma hiyo kufanya miamala ya kibenki bila kuwa na ulazima wa kufika kwenye tawi la benki husika na hivyo kupunguza usumbufu wa foleni na gharama za muda na nauli.

Benki zitakazohusishwa kwenye kammpeni hiyo ni pamoja na CRDB, ACB, Amana Bank, Benki ya Posta, NMB na Stanchat ambapo watoa huduma ya M-pesa watakuwa wakitoa elimu kwa wateja wanaotembelea matawi ya benki hizo ya jijini Dar es salaam.

Miongoni mwa miamala ambayo mteja wa M-pesa anaweza kuifanya kupitia simu ya mkononi ni pamoja na kuhamisha fedha kutoka akaunti ya M-pesa kwenda akaunti ya Benki, na kuhamisha fedha kutoka akaunti ya Benki kuja akaunti ya M-pesa na baadae kuweza kuitoa fedha hiyo kupitia wakala wa M-pesa mahala popote.

“Huduma ya M-pesa imewezesha huduma za kibenki kuwa popote bila kuwa na haja ya tawi la Benki, haya ni mafanikio makubwa ambayo tungependa wateja wetu wayafurahie na waone matunda ya kuwa katika mtandao wenye tofauti kubwa na mingine.”Alisema Mkurugenzi Mtendaji wa Vodacom Tanzania Rene Meza

“Kampeni yetu ya M-pesa benki popote pamoja na mambo mengine inalenga kuhakikisha kila mteja wa M-pesa ambae pia ana akaunti kwenye moja ya benki zinazotumia huduma hii anakuwa na uelewa na ufahamu wa kutosha juu ya namna ya kuitumia M-pesa kupunguza gahrama na usumbufu, na ndio maana tumeamua kutoa elimu hiyo kwenye matawi ya benki tukianzia jijini Dar es salaam.”Aliongeza Meza

Meza amesema kuwa M-pesa imerahisisha maisha kwa kiwango kikubwa na kwamba urahisi huo lazima umfikie kila mteja wa M-pesa wakati kampuni hiyo ikiendelea kuongeza kasi ya ubunifu kuiwezesha huduma ya M-pesa kuwa na mambo mengi zaidi yanayoleta maana na utofauti kubwa katika azima ya kuyaleta maisha viganjani.

“Huduma ya M-pesa imekuwa ikishamiri na kukua kwa kasi. Chachu kubwa ya mafanikio hayo ni  utofauti katika ubora, usalama na uhakika wa upatikanaji wake kupitia mawakala zaidi ya 40,000 nchi nzima, na hivyo kuvutia watoa huduma wengi nchini kuitumia huduma hii kama njia rasmi ya malipo ama kukusanyia michango, kodi na tooz mbalimbali na hivyo kurahisha upatikanaji wa huduma.”Aliongeza Meza



Mteja wa M-pesa anaweza kufanya miamala na makampuni zaidi ya 200 kupitia huduma ya M-pesa ikiwemo kuweka ama kutoa fedha kutoka kwenye akaunti yake ya benki au kutumia mtaandao wa mashine za ATM za baadhi ya benki kutoa fedha kutoka kwenye akaunti ya M-pesa.

Tangu ilipoanzishwa kwa mara ya kwanza nchini mwaka 2007 huduma ya M-pesa imekuwa mkombozi kwa wananchi kwa kurahisisha maisha ikiwa ni ya pili duniani kwa kuwa na idadi kubwa ya watumiaji na ya kwanza kutumia teknolojia ya kisasa zaidi ya huduma za fedha kupitia simu za mkononi ya R9.

Ni kupitia huduma ya M-pesa pekee ambapo simu ya mkononi huweza kumuunganisha mtu na makampuni zaidi ya 200 na hivyo kuwa na uwezo wa kukamilisha mahitaji yake mbalimbali akiwa mbali na watoa huduma mathalani malipo ya LUKU, Ving’amuzi vya Televisheni, tiketi za safari za anga,, ada ya shule, kununua muda wa hewani wa maongezi wa simu ya mkononi, kulipa kodi, kulipia bima n.k




Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.