Airtel yaongeza muda vifurushi vya Airtel Yatosha, sasa huduma masaa 25 kwa siku


  Airtel Tanzania imeendelea kutimiza dhamira yao ya kuwapatia wateja wake unafuu zaidi kupitia huduma yake ya AIRTEL YATOSHA nchini ambapo sasa wateja watafurahia Vifurushi vya Airtel Yatosha kwa masaa 25 kwa siku,   hii itawawezesha watanzania kufurahia kupiga simu mtandao wowote kwa gharama nafuu kwa muda mrefu zaidi.

Akiongea wakati wa uzinduzi wa Airtel yatosha masaa 25 Meneja Uhusiano wa Airtel Jackson Mmbando alisema” kuanzia sasa, huduma ya Airtel yatosha kwa siku itakua kwa masaaa 25 kuanzia pale mteja anapojiunga na huduma, yaani masaa 24 ya kuongea na kama vile haitoshi Airtel yatosha inakuongezea saa jingine moja la ziada. Sasa wateja wa Airtel watafurahi kupiga simu kwa gharama nafuu na kwa muda zaidi kuliko ilivyokuwa awali”.

 “Hii ni ya kwanza na pekee kutoka Airtel, Airtel yatosha itaendelea kuwa suluhisho la mawasiliano ya huduma za simu kwa watuamiaji na wateja wa Airtel nchi nzima ”. aliongeza Mmbando

Airtel yatosha ni huduma iliyoanzishwa ili kuleta kuvunja mipaka kwa watanzania na kuwawezesha kuwasiliana ndani na nje ya mtandaa kwa gharama nafuu. Kujiunga na huduma hii  piga *149*99# na atapata majibu papo hapo achague unataka Yatosha WIKI au Yatosha SIKU au Tosha ya Mwenzi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI