AKAMATWA KWA KUIBA STULI YA MWENGE WA UHURU

Saturday, June 8, 2013
ARUSHA, Tanzania
JIJI la Arusha limeendelea kujijengea sifa ya kuwa moja ya maeneo yenye vituko, kufuatia kijana mmoja mkazi wa eneo la Phillips, kata ya Sekei jijini humo, Hamad Rashid (32) kukamatwa leo akiiba kiti (stuli) kinachotumika kuwekea mwenge wa Uhuru wakati mwenge ukiwa katika mbio zake mkoani Arusha.

Tukio la kuiba na kisha kukamatwa limetokea jana saa 11 jioni katika eneo la Sanawari Mataa eneo lililopangwa kwaajili ya mkesha wa mwenge huo baada ya kukamilisha mbio zake na kazi ya kuweka mawe ya msingi na uzinduzi wa miradi mbalimbali ya maendeleo.

Kamanda wa polisi mkoa wa  Arusha Liberatus Sabas ameithibitishia Nkoromo Blog kutokea tukio hilo na kwamba mtuhumiwa huyo alikamatwa na polisi waliokuwa wakiulinda mwenge pamoja na kiti hicho.

Alisema tukio hilo lilitokea wakati mwenge huo pamoja na wakimbizaji wake kitaifa, kimkoa na viongozi wengine wakiwa katika harakati za usomaji wa salamu za utii kwa Rais, kabla ya kutangazwa ratiba ya mkesha.

Alisema kabla ya kukamatwa kwa mtuhumiwa huyo alionekana kumda mrefu akiwa amesogelea gari lililokua limebeba kiti hicho cha akiba bila kujua kwamba kulikua na askari waliokua wakimfuatilia nyendo zake.

Alisema muda mfupi askari huyo mwanamke alimuona kijana akisogelea zaidi gari na kuingiza mkono kisha kuchomoa kiti hicho kwa lengo la kuondoka nacho ambapo alishuka na kuanza kunyang’anyana nae kiti hicho.

“unajua ni ngumu hata kueleza maana mtu na akili zake anafanya namna hiyo hicho kiti kilikua ni cha akiba na kilikua ndani ya gari la wazi la mamlaka ya maji ambalo ndani yake kulikua na askari ambae alimuona huyo na hata alivyotakiwa kukiacha aliking’ang’ania na kuanza kunyang’anyana hadi askari wengine wakisaidiana na mgambo walipotokea”alisema Kamanda Sabas.

Alisema mara baada ya kukamatwa alihojiwa na polisi waliomkamata ambapo alijibu kuwa alikua anataka kukiangalia tu na haikua nia yake kukiiba na kuomba msamaha lakini, polisi wanaendelea kumuhoji ili kubaini nia yake hasa ya kukichukua kiti hicho, na huenda alafikmishwa mahakamani.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.