BENKI YA NMB YA ZINDUA CHAP CHAP AKAUNTI KWA AJILI YA WATANZANIA WASIO NA AKAUNTI

Benki ya NMB imeendelea kuwa kinara katika kubuni na kuboresha huduma mbali mbali za kibenki, ili kuwawezesha wateja wake kupata unafuu na urahisi wa upatikanaji wa huduma za kibenki nchini Tanzania. 

Katika kulizingatia hili mwishoni mwa wiki Benki  ya NMB ilizindua akaunti ya Chap Chap ambayo kusudi kubwa ni kuwafikia wananchi wote kule waliko na kuwafungulia akaunti zao.

Kikubwa zaidi ni kwamba mteja ataweza kufungua akaunti papo hapo na kupata kadi yake ya kutolea fedha  ndani ya dakika  kumi
·         
Mambo muhimu zaidi ambayo mteja wa Chap Chap anaweza kufaidika nayo ni pamoja na:



  1. Kuona salio la akaunti yako popote ulipo
  2. Kuweka fedha na kutoa fedha kwa mawakala wa M- pesa
  3.  Kutuma fedha kwa wasio na akaunti mahali popote nchini kwa kutumia huduma ya Pesa Fasta
  4. Kununua vocha za muda wa maongezi kutoka kwenye mtandao wowote wa simu
  5. Kuchukua fedha hadi shillingi 1.000,000/= kutoka kwenye ATM
 Mh. Waziri wa fedha Dk William Mgimwa akichukuliwa alama za vidole na Ofisa mauzo ya Nje NMB Abdul Kandoro mara baada ya uzinduzi rasmi wa NMB chap chap akaunti mwishoni mwa wiki mkoani Dodoma.
 Ofisa Mtendaji Mkuu wa Benki ya NMB Mark Wiessing akimshukuru Mh. Waziri wa Fedha Dk. William Mgimwa mara baada ya kuzindua akaunti ya NMB Chap chap .
Sehemu ya maofisa wa NMB na wageni waalikwa kwenye uzinduzi huo.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.