CCM MKOA WA DAR ES SALAAM, WATETA NA UJUMBE WA VIETNAM LEO
Na Pius Ntiga, UHURU FM
Chama Cha Kikomunisti Cha Vietnam-CVP, kimekitaka Chama Cha
Mapinduzi-CCM, kutoogopa kuwafukuza uanachama wake wasio na nidhamu
ambao hawazingatii maadili na kanuni za Chama kilichpo Madarakani.
Pia Chama hicho cha CVP kimesisitiza kuwa ni bora kuwa na
wanachama wachache kuliko kuwa na wanachama wengi wasio na nidhamu.
Kauli hiyo ya Chama cha Kikomunisti Cha Vietnam, imetolewa
leop Juni, 8, 2013 na Kiongozi wa Ujumbe wa Kamati Kuu ya Chama hicho
Bwana HOANG BINH QUAN wakati wa mazungumzo na uongozi wa Chama Cha
Mapinduzi-CCM Mkoa wa Dar es salaam ambao umeongozwa na Mwenyekiti wake
Ramadhan Madabida.
Katika mazungumzo hayo, Bwana QUAN pamoja na mambo mengine
amesisitiza umuhimu wa Chama cha siasa kudumisha nidhamu ndani ya Chama
na kuachana kabisa na kasumba ya kuwa na wanachama wengi huku miongoni
mwao wakiwa ni wasaliti wakubwa ndani ya Chama.
Kwa sababu hiyo Bwana QUAN akakiomba Chama Cha Mapinduzi
ambapo katika mazungumzo yao yalihuidhuliwa pia na Katibu wa NEC,
Itikadi na Uenezi NAPE NNAUYE kutowaonea haya wanachama wasaliti ndani
ya Chama.
Hata hivyo Chama Cha Mapinduzi-CCM kupitia kwa Katibu wake
Mkuu ABDULRAHMAN KINANA, tayari kilishatoa kauli kama hiyo ya kuwa ni
bora kuwa na wanchama wachache wenye nidhamu kiliko kuwa na wanachama
wengi wasio na nidhamu.
Kwa upande wake Mwenyekiti wa CCM, Mkoa wa Dar es salaam
Ramadhan Madabida ameuambia ujumbe wa Chama hicho cha Kikomunisti Cha
Vietnam kuwa CCM itaendelea kudumisha uhusiano wa siku nyingi na Chama
hicho huku akisistiza umuhimu wa wananchi wa Vietnam kuja kuwekeza
nchini hasa katika Mkoa wa Dar es salaam kutokana na fursa mbalimbali
zilizopo.
Pia pamoja na mambo mengine amezungumzia haja ya vyama hivyo
viwili vya CCM pamoja na CVP kubadilishana wanachama kwa kwenda
kujifunza namna mbalimbali za Kiuongozi ndani ya vyama hivyo.
Madabida ameainisha maeneo machache ya uwekezaji katika jiji
la Dar es salaam kuwa ni pamoja na eneo la uvuvi kupitia Bahari ya
Hindi, kilimo pamoja na sekta ya umeme hivyo akaomba wawekezaji kutoka
Vietnam kuja kuwekeza Tanzania.
Akishukuru kwa niaba ya Chama Cha Mapinduzi kuhusiana na ugeni
huo Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi NAPE NNAUYE amesema ujio wa
viongozi hao umefungua ukuraa mpya wa ushirikaino katika Nyanja
mbalimbali za kisiasa hasa ikizingatiwa historia ya muda mrefu kati ya
CCM na CVP.
Katika kusisitiza umuhimu wa ushirikiano huo Nape amesema CCM
daima itaendelea kushirikiana na Chama cha CVP kutokana na misingi
iliyoachawa na Rais wa Kwanza wa Tanzania Hayati Mwalimu Julius Nyerere
pamoja na Rais wa Kwanza wa Vietnam HO CHI MIHN.
Mazungumzo hayo yamehudhuriwa pia na Afisa wa Uhusiano wa
Mambo ya Nje wa CCM Makao Makuu Bi.Juliana Chitinka, Kaimu Katibu wa CCM
Mkoa wa Dar es salaam Ernest Charle, Katibu Msaidizi wa CCM Mkoa wa Dar
es salaam Silvester Mrope pamoja na Mwenyekiti wa CCM wilaya ya
Kinondoni Salum Madenge.
Ujumbe huo wa Chama Cha Kikomunisti Cha Vietnam-CVP, umemaliza
ziara yake ya kichama hapa nchini na ulitarajiwa kuondoka kurejea
nchini kwao Vietnam leo mchana.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (aliyesimama) akifunga mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramdahani Madabida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Viatnam, kwenye Ofisi za CCM mkoa wa Dar es Salaam, leo.
Mjumbe wa Chama Cha bKimomunisti cha China, akimpa zawadi Madabiba baada ya mazungumzo yao.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Madabida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi, Nape Nnauye (aliyesimama) akifunga mazungumzo kati ya Mwenyekiti wa CCM mkoa wa Dar es Salaam, Ramdahani Madabida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Viatnam, kwenye Ofisi za CCM mkoa wa Dar es Salaam, leo.
Mjumbe wa Chama Cha bKimomunisti cha China, akimpa zawadi Madabiba baada ya mazungumzo yao.
Katibu wa NEC, Itikadi na Uenezi Nape Nnauye, Madabida na Mjumbe wa Kamati Kuu ya Chama Cha Kikomunisti cha Vietnam wakiwa katika picha ya pamoja na viongozi wengine
Comments