CCM UINGEREZA WAGUSWA NA MLIPUKO WA BOMU ULIOTOKEA ARUSHA HIVI KARIBUNI


SALAMU ZA RAMBIRAMBI KUFUATIA MLIPUKO WA BOMU JIJINI ARUSHA 
Chama cha mapinduzi Tawi la Uingereza kwa masikitiko makubwa tunapinga vikali tukio la kurushwa bomu katika mkutano wa hadhara wa chadema uliofanyika jijini Arusha hivi karibuni na kusababisha vifo vya watu watatu na zaidi ya watu 40 kujeruhiwa. Tunatoa pole zetu za dhati kwa familia za wafiwa na kwa wale wote waliojeruhiwa katika janga hili la kikatili na kuwatakia uponaji wa haraka. Tukio hili limefuata badala ya lile la awali lililotokea katika kanisa katoliki la mtakatifu Joseph mnamo tarehe 5 mei mwaka huu jijini Arusha, ambapo pia lilisababisha vifo vya watu watatu na kujeruhi zaidi ya watu 60.

 Ni imani yetu kwamba uchunguzi kamili wa mashambulio haya utakamilika haraka na wahusika watakamatwa na kufikishwa mbele ya mkono wa sheria. Tanzania ni nchi yenye hazina ya amani ya muda mrefu. Vitendo vya kigaidi vya aina hii na ambavyo vina mlengo wa kutugawanya kamwe havitavumiliwa na vikomeshwe ili kuondoa wimbi la vurugu zinazoweza kusababisha uvunjikaji wa amani. Tunawasihi Watanzania wote tuwe pamoja na wenye busara na kuondokana na itikadi zozote za kisiasa au ushabiki wa vikundi , aidha na maneno ya kujibizana pasipo sababu.

Ili kuondoa ama kutoamsha hisia za chuki zisizo na manufaa kwa yeyote yule na Taifa kwa ujumla , ni vyema wakati wa majanga kama haya kuachia vyombo vya usalama kufanya kazi yake ya uchunguzi bila kuingiliwa na vyama au kundi lolote kwa maslahi binafsi au umaarufu wa kisiasa . Tunawasihi WaTanzania tuienzi amani yetu iliyolelewa kwa kipindi kirefu na Waasisi wa Taifa letu wakiongozwa na Hayati Baba wa Taifa Mwalimu Nyerere. Amani ambayo ni mfano na hadaa kwa wapenda amani kote ulimwenguni.

Imetolewa na idara ya Itikadi Siasa na Uenezi CCM UINGEREZA – UK.

MERGEFORMATINET TAWI LA UINGEREZA – UNITED KINGDOM Website ccmuk.org, Blog ccmuk.org/blog, Facebook page chama cha mapinduzi uingereza, twitter CCMUK 1 Contacts Phone +44 74 04 863333, E-mail – itikadi-uenezi@ccmuk.org

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.