CHAMA KIPYA CHA 21 CHA SIASA NCHINI TANZANIA CHAPATA USAJILI WA KUDUMU LEO KINAITWA CHAUMMA

Baadhi ya wanachama cha CHAUMMA pamoja na viongozi wao wakishangilia baada ya kupewa usajili.

Msajili wa Vyama vya Siasa Nchini, John Tendwa (kulia) akizungumza na wana CHAUMMA.
Tendwa akikabidhi cheti cha usajili CHAUMMA.
Wanachama wakionesha cheti cha usajili kwa wanahabari.
Gari la Mwenyekiti wa muda wa CHAUMMA, Wallance Mayunga, likiondoka baada ya hafla ya usajili.
Na  Thehabari.com

MSAJILI wa Vyama vya Siasa nchini, John Tendwa amekipa usajili wa kudumu Chama cha Ukombozi wa Umma (CHAUMMA) huku akivitaka vyama vya siasa kufuata sheria na kuepuka kuwa vyanzo vya vurugu na uchochezi wa migogoro.


Tendwa ameyasema hayo leo jijini Dar es Salaam alipokuwa akiwakabidhi cheti cha usajili wa kudumu viongozi wa chama kimpya cha kinachojulikana kama Chama cha Ukombozi wa Umma.


Alivitaka vyama vya siasa kuhakikisha vinatimiza malengo yao ya kushika dola na hata kama itashindikana kwao, basi kuhakikisha wanapata nafasi za uwakilishi wa wananchi zikiwemo za udiwani, ubunge pamoja na uongozi wa serikali za mitaa kwa mujibu wa taratibu za nafasi hizo.


Alisema kwa sasa vipo vyama vya siasa ambavyo licha ya kuwa na usajili wa kudumu na uongozi mzuri usio na migogoro vimeshindwa kutimiza malengo ya msingi ya chama kwa kushika nafasi za uwakilishi maeneo anuai kwa mujibu wa utaratibu.



“…Vyama hivi unakuta hawana mbunge, hawana diwani, hawana viongozi serikali za mitaa, kijiji na kwingineko lakini ukiangalia wana viongozi wazuri hawana migogoro ndani ya chama, haya sio madhumuni ya chama cha siasa,” alisema Tendwa.


Aidha aliwataka viongozi wa CHAUMMA kuhakikisha wanajipanga vizuri ili waweze kutimiza malengo ya chama na kuwawakilisha wananchi maeneo mbalimbali ya uongozi kisiasa. Alisema katika mapendekezo mapya ofisi yake inafikiria kuanza kuvipunguza vyama ambavyo licha ya kuwa na usajili havifanyi chochote kama ilivyo kwa madhumuni ya kuanzisha chama.


“Sheria inafanyiwa marekebisho, chama kikikaa ndani ya miaka mitano hakijafanya chochote tunafikiria kukifuta, kiongozi wa chama akitukana miezi sita unafungiwa kwa muda…maana hatuwezi kuruhusu matusi, vurungu na masuala mengine yasiokuwa na msingi ndani ya vyama vya siasa,” alisema Tendwa.


Hata hivyo amesema katika mapendekezo yao ya mabadiliko ya katiba wamependekeza mambo mengi ikiwemo sasa kuruhusu vyama kujiunga na kufanya shughuli za siasa kama ilivyo kwa nchi za Kenya, Afrika Kusini, Lethoto na nchini Namibia.


Akizungumza mara baada ya kukabidhiwa cheti cha usajili wa kudumu Mwenyekiti wa muda wa CHAUMMA, Wallance Mayunga alisema wamejipanga vizuri katika kuwatumikia wananchi na chama chake kinatambua changamoto zilizopo nchini katika uongozi, utendaji na utawala hivyo kina nia ya kuleta mabadiliko.


Nafasi ya Katibu Mkuu wa muda wa CHAUMMA inashikiliwa na Shaffii Abed huku Hamad Tao akiwa ni miongoni mwa wanachama waanzilishi wa nchama hicho.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.