KAMBI YA MISS KINONDONI YAZINDULIWA RASMI, YAANZISHA HARAMBEE YA KUNUA VITANDA HOSPITALI ZA MWANANYAMALA NA SINZA PALESTINA

      
Naibu Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Songolo ambaye alimwakilisha mgeni rasmi meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda akiongoza harambee ya kuchangisha fedha kwa ajili ya kununua vitanda kwa ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds) kwa hospitali za Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina ambapo warembo hao walitembelea wodi za akina mama na kufanya usafi. Pamoja na harambee kulizinduliwa rasmi kambi ya Redds Miss Kinondoni 2013. Pembeni ni Mkuu wa Itifaki wa Mashindano ya Miss Tanzania, Albert Makoye na Mratibu wa shindano la Redd’s Miss Kinondoni Bw. Ssebo. Harambee hiyo ilifanyika ukumbi wa Ambassador uliopo hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam. 
Jumla ya vitanda 15 vyenye thamani ya shilingi milioni 52.5 zimepatikana katika harambee iliyoandaliwa na warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 kwa ajili ya kununua vitanda kwa ajili ya akina mama wanaojifungua (delivery beds) kwa hospitali za Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina iliyofanyika katika ukumbi wa Ambassador uliopo hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam. 

Akizungumza mshiriki wa shindano hilo, Sarah Paul alisema kuwa wanamshukuru Mungu kwa kuweza kuwawezesha kufanya harambee hiyo ambayo ilitokana na wao baada ya kutembelea hospitali ya Mwananyamala pamoja na Sinza Palestina wakajionea uhaba wa vitanda vya akina mama wakati wa kujifungua.

“Tulisononeshwa sana na hali tuliyoikuta hospitalini hapo ambapo baada ya kuongea na mganga mkuu wa Manispaa ya Kinondoni dokta Gunini Kamba alitueleza kuwa jumla ya akina mama wapatao 50 mpaka 80 hujifungua kwa siku moja hivyo wanauhaba wa vitanda, tukaona tukae na viongozi wetu watusaidie kuandaa harambee na tunamshukuru Mungu tumefanikiwa kupata vitanda 15 japo nia yetu ilikuwa ni kupata vitanda 20,” alisema mrembo huyo.

Mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni 2013 yanatarajia kufanyika kwenye ukumbi wa hoteli ya Golden Tulip siku ya Ijumaa 21 June 2013. Viingilio katika onyesho hilo ni shs. 60,000 VIP, shs. 25,000 kwa tiketi za kawaida na meza ya watu ukitazama zawadi.
Warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 wakitambulishwa kwa Naibu Mustahiki Meya wa Manispaa ya Kinondoni Mheshimiwa Songolo ambaye alimwakilisha mgeni rasmi meya wa Manispaa ya Kinondoni, Yusuph Mwenda. Mgeni huyo pia alipata fulsa ya kuzinduliwa rasmi kambi ya Redds Miss Kinondoni 2013 iliyopo katika hoteli ya JB Belmont jijini Dar es Salaam. 
Warembo wa Redds Miss Kinondoni 2013 walipata fulsa ya kucheza mara baada ya harambee na ufunguzi rasmi ya kambi yao. 
Furaha zilitanda.
Kila mmoja akionyesha ufundi wake.
Mashindano ya Redd’s Miss Kinondoni yamedhaminiwa na Redd’s Original, Chilly Willy Energy Drink, Oriflame Natural Beauty Products, Times Fm, JB Belmonte Hotel, Michuzi Media Group, Michuzijr Blog, Mtaa Kwa Mtaa Blog, Fullshangwe Blog, HandeniKwetu Blog, Mrokim Blog, TheHabari.com, JestinaGeorge Blog, SufianMafoto Blog, Global Publisher, Mdimuz Blog, Lukaza Blog, MO Blog na Kajunason Blog.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*