KANDORO AWAKABIDHI HATI MILIKI ZA MASHAMBA WAKULIMA WA CHAI RUNGWE MKOANI MBEYA

Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akihutubia wananchi wa kijiji cha Ntandabala kata  ya Masoko Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wakati wa  hafla ya kugawa Hati Miliki kwa wakulima wa Chai iliyofanyika katika viwanja vya Tarafa ya Pakati.
Mkuu wa Mkoa wa Mbeya AbbaS Kandoro akiwa na baadhi ya Viongozi wa Wilaya ya Rungwe wakiongozwa na Mkuu wa Wilaya hiyo Crispin Meela wakati wa  hafla ya kugawa Hati Miliki kwa wakulima wa Chai iliyofanyika katika viwanja vya Tarafa ya Pakati.







Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akimkabidhi  mwananchi wa kijiji cha Ntandabala kata  ya Masoko Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wakati wa  hafla ya kugawa Hati Miliki kwa wakulima wa Chai iliyofanyika katika viwanja vya Tarafa ya Pakati.
Mkuu wa mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro akisalimiana na mwananchi wa kijiji cha Ntandabala kata  ya Masoko Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya wakati wa  hafla ya kugawa Hati Miliki kwa wakulima wa Chai iliyofanyika katika viwanja vya Tarafa ya Pakati.
 Baadhi ya wananchi wakifuatilia kwa makini zoezi la ugawaji hati miliki za mashamba kwa wakulima wa Chai Wilayani Rungwe.
 Ngoma za asili ya Wanyakyusa zikitoa burudani uwanjani hapo

MKUU wa Mkoa wa Mbeya Abbas Kandoro ameziagiza Halmashauri za Wilaya kutengeneza mipango mizuri ya matumizi bora ya Ardhi vijijini ili kuepusha  migogoro ya mara kwa mara ikiwa ni pamoja na kutenga bajeti kwa ajili ya kusaidia zoezi la upimaji.
Hayo aliyasema juzi katika hafla ya kugawa Hati ya Haki miliki za Ardhi za kimila kwa wakulima wa Chai iliyofanyika katika viwanja vya makao makuu ya Tarafa ya Pakati iliyopo  katika Kijiji cha Ntandabala kata ya Masoko Wilaya ya Rungwe Mkoani Mbeya.
Kandoro alisema ili kuepusha migogoro inayotokana na ardhi ni vema Halmashauri ikatengeneza mpango wa matumizi bora ya ardhi kama kutenga eneo lawazi, shule, zahanati na maeneo ya kupitisha miundombinu mapema kabla ya kuanza kuwagawia wananchi.
Aidha amewasihi Wakulima kuhakikisha wanazitunza vizuri Hati miliki walizopewa kwa kuogopa kutapeliwa na watu wengine ambao wanaweza kuwanyang’anya hadi mashamba yao na wao kuishia kuwa maskini kutokana na kutokuwa na haki na ardhi yake.
“ Hakikisheni mnazitunza vizuri kuepuka matapeli, pia chukueni Hati hiyo kama kielelezo kinachokuhakikishia kuwa wewe ndiye mmiliki halali wa ardhi hiyo popote utakapokuwepo pia yatunzeni na kuyaendeleza maeneo hayo” alisema Mkuu huyo wa Mkoa.
Aliongeza kuwa Hati Miliki pia husaidia kuepusha migogoro ya mirathi na kunyanyaswa kwa wajane  kutokana na kuwepo kwa Hati inayoonesha mmiliki halali wa Ardhi hiyo.
Kwa upande wake Mkuu wa Wilaya ya Rungwe Crispin Meela akitoa taarifa kwa Mkuu wa Mkoa wa Mbeya alisema Jumla ya wananchi 400 wameitikia wito wa kupimiwa ardhi na kukabidhiwa hati miliki zao hivyo kuwafanya kuishi maisha bora kama Ilani ya Chama cha Mapinduzi inavyotaka.
Meela alisema mradi wa upimaji wa mashamba kwa wakulima hao umefanywa na Mpango wa Kurasimisha Rasilimali na Biashara za Wanyonge Tanzania( Mkurabita)na kwamba jumla ya vijiji saba vimenufaika ambavyo ni Bujela, Nsongole, Njugilo, Kyambambembe, Nsyasya, Ntandabala na Bulongwe.
Naye Mratibu wa Mradi wa Mkutabita Gwabo Mwansasu alisema Mradi huo umeanza kutekelezwa Novemba Mwaka jana kwa awamu mbili ambapo mchakato wa awamu ya kwanza ulianza kufanyika mwaka 2004/2005 kwa ufadhili wa Abbott Axio ikiwa na lengo la kuwasaidia wajane na watoto yatima wa kata ya  Kinyala kumiliki ardhi yao.
Aliongeza kuwa awamu ya pili ilitekelezwa na Wizara ya Ardhi Nyumba na Maendeleo ya Makazi kwa ufadhili wa European Union Mwaka 2007/2008 kwa vijiji 16, ambapo Vijiji 8 kutoka Rungwe Mashariki na Vijiji 8 kutoka Rungwe Magharibi.
Mwansasu alisema katika Mradi wa sasa wa awamu ya tatu umetekelezwa na Mkurabita kwa kushirikiana na Bodi ya Chai Tanzania pamoja na wakala wa maendeleo ya Wakulima wadogo wa Chain a lengo likiwa ni kupima mashamba ya Chai.
Alisema Mradi huu wa uwezeshaji wakulima wa Chai skimu ya Segera inayojumuisha vijiji 19 vya Masukulu, Kyambambembe, Segera, Mpombo, Ijigha, Ntandabala, Matwebe, Busisya, Bulongwe, Mpumbuli, Nsongola, Nsyasya, Bujela, Njugilo, Lufumbi, Kasyeto, Igembe, Kiloba na Ngaseke.
Mratibu huyo aliongeza kuwa Mradi huo ulianza Novemba 19, Mwaka  2012 na kukamilika Juni 15, Mwaka huu ambapo umegharimu Shilingi 64,078,440/= kwa awamu mbili fedha zilizotolewa na wafadhili.
Alisema Jumla ya mashamba ya wakulima 1891 yenye ukubwa wa Hekta 485.12 yamepimwa na kutolewa hati miliki za kimila 400 zenye ukubwa wa Hekta 160.45 kwa vijiji saba.

 Na Mbeya yetu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.