Kila la kheri Taifa Stars: Nape.

Chama Cha Mapinduzi (CCM) kimeitakia kila la kheri timu ya Taifa Stars ambayo inacheza  kutafuta tiketi ya kucheza kombe la dunia mwaka 2014.
Taifa Stars katika mechi yake ya kesho itavaana na Timu ya taifa ya Morocco. 
Akizungumza kutoka Dar es salaam ,Katibu wa NEC Itikadi na Uenezi Ndg. Nape Nnauye alisema CCM inaitakia kila lakheri Taifa Stars na mafanikio katika mchezo wa kesho na kwamba CCM inatambua umuhimu wa taifa Stars kushinda mechi hiyo ya kesho.
Alisema anaamini dua za CCM na Watanzania wote zitaiwezesha Taifa Stars kushinda mechi yake dhidi ya Morocco. "Watanzania tunaomba muiombee Taifa Stars, tunaimani nayo, bila shaka itashinda kesho" alisisitiza Nape
Nape Moses Nnauye
The CCM Secretary for Ideology & Publicity

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU