MAKAMU WA RAIS DKT. BILLAL AONGOZA KILELE CHA SIKU YA MAZINGIRA KITAIFA NAMANYERE MKOANI RUKWA
Makamu
wa Rais wa Jamhuri ya Muungano wa Tanzania Mhe. Dkt. Mohammed Gharib
Billal akihutubia wananchi katika viwanja vya sabasaba Mji mdogo wa
Namanyere Mkoani Rukwa katika kuhitimisha siku ya mazingira duniani
ambayo kitaifa imefanyika Mkoani Rukwa jana tarehe 05.06.2013. Katika
hotuba yake hiyo alisisitizia juu ya uhifadhi wa mazingira kwa kutunza
vyanzo vya maji, milima na misitu ya asili, kuhifadhi ardhi na kupanda
miti katika maeneo yaliyoathirika na usafi wa mazingira kwa ujumla.
Makamu
wa Rais Dkt. Mohammed Gharib Billal akikagua kitalu cha miche ya miti
mbalimbali ya mjasriamali ndugu Kidevu (kushoto) katika maonyesho kwenye
kilele cha siku ya mazingira kitaifa Mkoani Rukwa katika Mji mdogo wa
Namanyere wilayani Nkasi jana tarehe 05.06.2013, Kulia ni Waziri wa Nchi
Ofisi ya Makamu wa Rais-Mazingira Dkt. Terezya Luoga Huvisa.
Comments