MAVETERANI WAONESHANA UBABE UKONGA!

Mbunge wa Jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa akikagua timu za Kigogofresh na Tumaini kabla ya kuanza kwa mpambano wao kwenye bonanza la Maveterani lililoandaliwa na mbunge huyo mwishoni mwa wiki eneo la Pugu Kajiungeni jijini Dar es Salaam mwishoni mwa wiki, matokeo ya mchezo huo Kigogo ilishinda 2 kwa 1.
Mbunge wa jimbo la Ukonga  Eugene Mwaiposa akimkabidhi jezi kapteni wa  timu ya vijana wa CCM wa jimbo hilo Abubakari (fulana ya bluu) wakati walipoalikwa kwenye bonanza la maveterani wa jimbo hilo.
Wazee wa jimbo la Ukonga wakipambana kumkamata kuku wakati wa bonanza la jimbo hilo mwishoni mwa wiki.
Wazee wa jimbo la Ukonga wakipambana kumkamata kuku wakati wa bonanza la jimbo hilo mwishoni mwa wiki.
Tulia hapa!
Mwenyekiti wa Serikali ya mtaa wa Bombani Pugu akishangilia mara baada ya kukamata kuku aliyeshindaniwa na Wazee wa eneo hilo ikiwa ni miongoni mwa michezo iliyofanyika kwenye bonanza lililoandaliwa na mbunge wa jimbo la Ukonga Eugene Mwaiposa mwishoni mwa wiki.
BONANZA la Maveterani jimbo la Ukonga limefanyika mwishoni mwa wiki na kushuhudia maveterani waalikwa kutoka Sinza timu yenye Star wengi wa zamani ya Golden Bush wakiibuka mabingwa wa mchezo wa Soka.
Bonanza hilo lililoandaliwa na Mbunge wa Jimbo hilo Eugene Mwaiposa lilizikutanisha timu zipatazo kumi za jimbo hilo na timu mbili zilialikwa kwenye Bonanza hilo.

Ushindani kwenye michuano hiyo ulikuwa mkali ambapo wenyeji wa mashindano hayo timu ya Pugu ilitinga fainali na kupambana na timu ya Golden Bush ya Sinza iliyojaza nyota kama Salum Sued Kusi, Abuu Mtiro na Amani Simba.
Hata hivyo haikuwa kazi rahisi kwa mastaa hao kupata ubingwa huo kwa vijana wa pugu hadi pale ilipofikia changamoto ya mikwaju ya Penalt 5, ambapo Golden Bush walipata Penalt saba kwa 6, kutokana na kumaliza muda wote wa mchezo bila kufungana.
Kivutio kikubwa kwenye bonanza hilo kulikuwa kwa mwanamuziki wa kizazi kipya KR Mulla, alipoingia kwa upande wa timu ya Golden Bush na kufanikiwa kuunganisha kross kali na kupiga bao ambapo alishangalia kwa Staili ya mapanga Shaa! na kurusha miguu juu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI