MH. ZITTO KABWE KUHUDHULIA TAMASHA LA ASPEN IDEAS 2013 NCHINI MAREKANI


MBUNGE WA Kigoma Kaskazini, Ndugu Zitto Z. Kabwe amealikwa kuhudhuria tamasha la tisa la Aspen la mwaka huu huko Marekani.  Tamasha hilo linawaleta pamoja watu mashuhuri kutoka nyanja mbalimbali duniani.

Lengo kubwa la tamasha ni kuwawezesha washiriki kubadilishana mawazo kuhusiana na masuala mbalimbali ambayo wana uzoefu nayo.Ushiriki katika tamasha hilo utamwezesha Zitto kukutana na kubadilishana  mawazo na magwiji wa masuaka mbalimbali duniani.

Ratiba iliyotolewa na waandaaji inaonyesha kuwa tamasha hilo litakaloendeshwa kwa muda wa wiki moja kuanzia Juni 26, limegawanyika  katika sehemu mbili. Kama ilivyo kwa miaka iliyopita, tamasha hilo litahusisha majadiliano ya pamoja, ya vikundi pamoja na ya mtu mmoja mmoja.

Pia washiriki watakuwa na fursa ya kukutana na wabunifu na wataalamu wa  nyanja mbalimbali na kubadilishana nao mawazo. Mijadala itahusu mambo ya kijamii, siasa, mahusiano ya kimataifa, watoto na vijana pamoja na namna ya kukabiliana na changamoto kubwa zinazoikabili dunia hivi sasa. Vile vile kutakuwa na maonyesho ya vitabu pamoja na mikutano na waandishi wa habari maarufu kutoka Marekani. Washiriki pia watapata
fursa ya kujifunza kupitia filamu na michezo ya kuigiza.

“Nimefurahi kupata mwaliko huu na nimekubali kushiriki kwa sababu
kwangu mimi hii ni nafasi adhimu sana na kupanua uelewa wangu wa
masuala mbalimbali, pia ni fursa kubwa ya kueleza maoni yangu kwa waalikwa mbali mbali.

Nina uhakika kuwa watu nitakaokutana na  kubadilishana nao mawazo na uzoefu watasaidia kupanua uelewa wangu wa masuala kadhaa”, alisema Zitto alipotakiwa kufafanua umuhimu wa  tamasha hilo kwa vijana.

Baadhi ya watu maarufu watakaotoa mada katika tamasha hilo ni pamoja na  Majaji washiriki wa Mahakama Kuu ya Marekani Stephen Breyer na  Elena Kagan, Mwakilishi Eric Cantor, Rais wa Kituo cha Brady Dan  Gross, Rais wa Chama cha Wamiliki wa Bunduki Marekani David Keene,

Balozi wa Marekani katika Umoja wa Mataifa Susan Rice; Rais wa Taasisi  ya Taasisi ya Kulinda Rasilimali, Frances Beinecke; Mkurugenzi mwenza wa Boies, Schiller & Flexner LLP David Boies, Waziri wa kazi wa zamani


Elaine Chao, Waziri wa Usafirishaji Ray LaHood, Meya wa New Orleans Mitch Landrieu, Waziri wa Fedha wa zamani Hank Paulson, Gavana wa zamani wa Minnesota Tim Pawlenty, Mshauri wa Chama cha Republican  Karl Rove na Rais wa Shirikisho la Walimu Marekani Randi Weingarten. Taasisi ya Aspen inajihusisha na masuala ya elimu na sera ambayo ina  makao makuu katika jiji la Washington, Marekani. Lengo lake kuu ni kuendeleza maadili ya kiuongozi. Pia taasisi hii ni kama kituo cha kuwezesha kutafuta ufumbuzi wa masuala magumu.

Taasisi ina matawi kadhaa baadhi yakiwa huko Aspen, Colorado na Wye River huko Maryland. Pia Taasisi ina ofisi katika jiji la New York. Pia taasisi  ina mtandao mkubwa wa washiriki duniani kote.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI

KOCHA WA AL.AHLY ASEMA YANGA NI TIMU BORA NA NGUMU