MWANAMKE MBEYA MATATANI KWA KUUA MUME KISA KUUZA KARANGA DEBE MOJA BILA KUSHIRIKISHANA

 
 
 
Na Esther Macha, Mbeya
MWANAMKE mmoja mkazi wa kijiji cha Iganduka wilayani Mbozi Mkoani Mbeya makrina Simbowe (42) anashikiliwa na jeshi la polisi Mkoani hapa kwa kosa la kumuua mumewe aitwaye Rodrick Mwaipasi (55)baada ya mwanamke huyo kuuza karanga debe mbili bila idhini ya mume wake.
Tukio la kifo cha mwanaume huyo linatokana na marehemu kuhoji kwa mke wake juu ya kuuza karanga debe mbili bila idhini yake na hivyo mwanamke huyo kumsukuma mume wake ambaye aliangukia kisogo na kufariki papo hapo.
Akizungumza na waandishi wa habari jana ofisini kwake Kamanda wa polisi Mkoani Mbeya Bw.Diwani Athuman alisema tukio hilo limetokea juni 24 mwaka huu majira ya saa 2.00 usiku katika kijiji cha Iganduka wilayani hapa
Baada ya marehemu kusukumwa alidondoka na kupelekwa katika hospitali mbozi mission ambapo hata hivyo alikuwa ameshafariki kutokana na kuangukia kisogo.

Aidha Diwani alisema chanzo cha mzozo huo ugomvi wa kifamilia uliotokea kati yao kisha marehemu kusukumwa na mke wake na kufariki dunia.

Hata hivyo Kamanda Athuman alisema kuwa mtuhumiwa amekamatwa na taratibu zinafanywa ili afikishwe mahakamani ,na kutoa wito kwa jamii kutatua matatizo/migogoro yao kwa njia ya mazungumzo badala ya kujichukulia sheria mkononi kwa kutumia hasira na nguvu.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

HAKUNA BINADAMU ALIYESALIMIKA NA UPOFU HUU...

SERIKALI KUWACHUKULIA HATUA WATANZANIA WATAKAOVAA JEZI ZA MAMELODI AU AL AHLY

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

KOCHA BENCHIKHA AMESEPA

MASHUSHUSHU WA MAMELODI WALIKUJA KUTUPELELEZA: HERSI