MWANDISHI TANZANIA DAIMA JAJI REDD'S MISS TANGA

Clezencia Tryphone 
Na Elizabeth John
MWANDISHI wa Tanzania Daima Clezencia Tryphone ‘Tasha’ anatarajia kuwa jaji katika shindano la kumsaka Redds Miss Tanga akisaidiana na aliyewahi kuwa Miss Tanzania miaka kadhaa iliyopita.
Tasha, anatarajia kufanya kazi pamoja na Miss huyo katika shindano hilo linalotarajiwa kutimua vumbi Juni 22 katika uwanja wa Mkwakwani Mjini humo.
Akizungumzia uteuzi huu uliofanywa na Kampuni ya Datk ambao ni waratibu wa Shindano hilo, Tasha alisema, amefarijika kupata nafasi hiyo ya kuwa jaji katika shindano hilo na kuaidi kufanya kazi vema na Wema ili waweze kumpata mrembo bora na mwenye vigezo.
Tasha alisema, licha ya kuwa ni mara yake ya kwanza kuwa jaji wa shindano hilo, amedai kuwa na uwezo na kazi hiyo kwa kuwa ni muumini mkubwa wa mashindano mbalimbali ya umis hapa nchini.
“Kwanza namshukuru mungu kwa uteuzi huu, naimani bila yeye mimi nisingepata nafasi hiyo, na nimaimani nitafanya kazi vizuri kwa kushirikiana na mwenzangu ili tuweze kumpata mrembo mwenye vigezo ambaye ataiwakilisha vema Redds Miss Tanga na kutwaa taji la Taifa,”alisema Tasha.
Tasha aliongeza kuwa mpaka sasa anaendelea na mafunzo ya ujaji ili aweze kufanya kazi yake kwa ufasaha bila ya kuwepo kwa upendeleo dhidi ya mtu yoyote.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.