NDOTO ZA USHINDI ZA MSAMBATAVANGU NA KINANA DHIDI YA KUKIGALAGAZA CHADEMA YATIMIA IRINGA

 katibu mkuu  wa CCM Bw Kinana akiagana na makada  wa CCM mkoa  wa Iringa  hivi karibuni
 Kada  wa CCM mjini Iringa Bw  Shukru Stivine  akisalimiana na katibu mkuu  wa CCM Taifa  Bw  Kinana  leo  mgombea  udiwani  wa  CCM kata ya Mbalamaziwa  wilayani Mufindi Bw  Zuberi  Nyomolela  wa  pili  kushoto , wa kwanza  kushoto ni mwenyekiti  wa CCM mkoa  wa Iringa Bi Jesca Msambatavangu na kutoka  kulia wa kwanza ni katibu mwenezi na itikadi Taifa  Nape Nnauye  na katibu mkuu  wa CCM Taifa  Bw Kinana
Diwani mteule wa kata ya Mbalamaziwa Mufindi aliyekisurubu vibaya  Chadema  Bw  Zuberi  Nyomolela  (kushoto) akiwana katibu mkuu  wa CCM Taifa Bw Kinana hivi karibuni  wakati akimnadi katika  kijiji  cha Mbalamaziwa


 Katibu mkuu  wa CCM Taifa  Bw Kinana akiwapongeza  wanachama wa CCM kata ya  Mbalamaziwa ambao  walishindwa katika mchakato wa kura za maoni katika kinyang'anyiro cha  udiwani ndani ya CCM kata  hiyo
......................................................................................................................................

AHADI iliyotolewa na Mwenyekiti wa Chama cha Mapinduzi (CCM) mkoa wa Iringa Jesca Msambatavangu kwa katibu mkuu wa chama hicho Taifa, Abdulaman Kinana  kwamba watakibwaga Chama cha Demokrasia na Maendeleo (Chadema) katika uchaguzi mdogo wa madiwani mkoani hapa, imekuwa kweli.
Msambatavangu alimueleza Kinana alipopita hivi karibuni mjini Iringa wakati akielekea mkoani Njombe kwa ziara ya kikazi kwamba CCM itapata ushindi wa kishindo kwenye uchaguzi huo katika kata ya Ng’ang’ange  wilayani Kilolo na Mbalamaziwa, wilayani Mufindi.
“Niliahidi na imekuwa kweli kwasababu kazi ya maendeleo inayofanywa na serikali ya CCM inazidi kurejesha imani kwa wananchi na inadhihirisha jinsi wanavyopuuza kelele za baadhi ya wanasiasa wanaopinga maendeleo yanayofanywa,” alisema

Akitangaza matokeo ya uchaguzi huo katika kata ya Ng'ang'ange, msimamizi msaidizi  wa uchaguzi huo, Esabela  Kamwela alisema jumla ya  wapiga kura  919 kati ya  1087 waliojiandikisha walishiriki uchaguzi huo.

Alisema Chadema ilimsimamisha Lucas Chahe huku CCM ikimsimamisha Nangamleki Yohanes katika  uchaguzi huo uliomaliza katika hali ya utulivu na amani.
Kamwela  alisema katika  uchaguzi huo kura 16 ziliharibika  huku mgombea wa Chadema akianguka  vibaya kwa  kupata  kura 217 na mgombea wa CCM akiibuka  kidedea kwa kuzoa kura 686.

Katika kata ya Mbalamaziwa ambako Chadema ilijipata matumaini ya ushindi kwa kile kilichoonekana mikutano yake kupata idadi kubwa ya watu, mgombea wake alibwagwa vibaya dhidi ya mgombea wa CCM.

Katika kata ya Mbalamaziwa ambako ni jirani kabisa na kata  ya Nyololo ambayo imeingia katika vitabu vya historia baada Septemba 2, mwaka jana wananchi wake kuhuhudia tukio ambalo halikuwahi kutokea katika nchi hii la mwandishi wa habari Daudi Mwangosi kuuawa wakati Chadema ikiendelea na harakati zake za kuimarisha chama chao,  mgombea  wake  Ezekiel Mlyuka aliambulia kura 185 tu kati ya kura 1,611 zilizopigwa.
Mgombea wa CCM, Zuberi Nyomolelo aliibuka mshindi wa kiti hicho cha udiwani baada ya kupata kura 1,426; kura  26 zikiharibika .

Katika mazingira ya kufurahisha, wagombea wa vyama vyote wameyakubali matokeo hayo, huku wafuasi wa CCM na wateule wao wakiendelea na shamrashamra wakisubiri siku ya kuapishwa kwa ajili ya kuwatumikia wananchi.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.