NSSF3
ILO NA TACAIDS WAENDESHA KONGAMANO LA KUJADILI MIKAKATI YA KUWAWEZESHA WANAWAKE, WASICHANA NA WAVULANA KIUCHUMI KATIKA HARAKATI ZA KUPUNGUZA HALI HATARISHI ZA MAAMBUKIZI YA UKIMWI NCHINI.
Mkurugenzi wa Shirika la Kazi Kanda ya
Afrika Mashariki nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo amesema
kupitia msaada kutoka Serikali ya Sweden wa kifedha ILO iliweza
kuwahusisha wasichana na wavulana katika makundi mbalimbali wenye vipato
vidogo kupata uelewa wa Afya ya Uzazi kupitia Makongamano, Semina na
Mafunzo mbalimbali yaliyoendeshwa na shirika hilo la kazi Duniani.
Ameongeza kuwa “tuliwasaidia
kuwaunganisha na vikundi vya kuweka na kukopa ili waweze kupata mitaji
midogo midogo ya kufungua biashara ndogo ndogo katika harakati za
kuwafanya wajitegemee na kuepekana na vishawishi vya Ngono isiyokuwa
Salama.
Bw. Musindo amesisitiza Umuhimu wa
TACAIDS kuandaa makongamano kama haya ili kuwawezesha wasichana na
wavulana wadogo kupata ufahamu uelewa na mafunzo ya uzazi wa Afya na
jinsi ya kuelewa mabadiliko yao ya kimaumbile.
“Ni matumaini yangu mwingiliano huu wa
Utamaduni wa kupambana na Ukimwi, Kinga na Uwezeshwaji wa Kiuchumi
umefanyika vizuri, hasa katika kuyalenga makundi yaliyo katika mazingira
magumu itasaidia kuongeza kasi ya kupunguza maambukizi mapya kama
ilivyoripotiwa na ripoti ya UNAIDS mwaka 2012 Duniani kwamba maambukizi
mapya yamepungua kwa Asilimia 20”. Amesema.
Sehemu ya washiriki wakifuatilia mada mbalimbali zilizowasilishwa leo kwenye Kongamano hilo.
Mgeni rasmi Katibu Mkuu wa Wizara ya
Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Kijakazi Mtengwa akizungumza kwa niaba ya
Waziri wa Wizara hiyo amesema mikakati ya kuwawezesha Wanawake Kiuchumi
inaweza kupunguza hatari ya kupata maambukizi ya Virusi vya Ukimwi kwa
Wanawake, Wasichana na Wavulana wadogo.
Amesema Jamii lazima itambue kuwa
juhudi zaidi zinahitajika ili nchini yetu iweze kufikia malengo ya 0.3
yaani Tanzania ambayo haina maambukizi mapya ya VVU, Ukimwi usiwe sababu
ya vifo, vile vile pasipo unyanyapaa wala ukatili kwa mtu yeyote
anayeishi na Virusi vya Ukimwi.
Mwenyekiti wa Tume ya Kudhibiti Ukimwi
(TACAIDS) Dr. Fatma Mrisho akizungumza na washiriki amesema Takwimu
zinazonyesha Wanawake wako katika hali ya hatari ya kuambukizwa zaidi
kuliko wanaume ambapo mpaka sasa ni Asilimia Sita ya Wanawake nchini
huambukizwa wakati wanaume ni Asilimia 3 nchini nzima.
Dr. Mrisho alisisitiza umuhimu wa
kumwezesha mwanamke kiuchumi kama ndio moja ya suluhisho la kumfanya
kutokuwa tegemezi katika jamii.
“Amesema takwimu zinazonyesha katika
nchi nyingi za Kiafrika umaskini unachagia sana kuenea kwa Ukimwi maana
Wanaume wengi hutumia umasikini wa Wasichana au Kinadada kuwarubini kwa
fedha na kufanya nao Ngono isiyosalama”.
Dr. Fatma Mrisho amepongeza juhudi za
ILO na kuwataka mashirika mengine na wadau wa mapambano dhidi ya Ukimwi
kuiga juhudi zilizofanywa na ILO za kuandaa makongamano ya kiuchumi ili
kumwezesha Mwanamke na wavulana wadogo kujitambua na kuelewa jukumu lao
katika mapambo ya VVU na Ukimwi nchini.
Meza Kuu: Kutoka kushoto ni Mkurugenzi
wa Shirika la Umoja wa Mataifa la Ukimwi Tanzania (UNAIDS) Dr. Hedia
Belhadj, Mwakilishi kutoka TUCTA Bw. Hezron Kaaya, Katibu Mkuu wa Wizara
ya Jamii, Jinsia na Watoto Bi. Kijakazi Mtengwa, Mwenyekiti wa Tume ya
Kudhibiti Ukimwi (TACAIDS) Dr. Fatma Mrisho, Mkurugenzi wa Shirika la
Kazi Kanda ya Afrika Mashariki nchini Tanzania (ILO) Bw. Alexio Musindo,
Mkurugenzi wa Sera na Utetezi wa Chama cha waajiri Tanzania (ATE) Bi.
Justina Lyela.
Mwakilishi kutoka shirikisho la
wafanyakazi Tanzania (TUCTA) Bw. Hezron Kaaya alisisitiza mshikamano na
umoja wa wafanyakazi katika mapambano ya VVU na Ukimwi sehemu za kazi.
Bw. Kaaya amesisitiza majadiliano kama
hayo yasiishie kwenye makabrasha bali wayatekeleze kwa vitendo ili
kuleta matokeo chanya kwenye jamii.
Mkurugenzi wa Sera na Utetezi wa Chama
cha waajiri Tanzania (ATE) Bi. Justina Lyela akitoa nasaha zake kuhusu
viwango sawa vya malipo ya mishahara kwa wafanyakazi nchini ili
kuwakomboa wanawake na kipato kidogo makazini.
Picha juu na chini ni sehemu ya
washiriki kutoka ndani na nje ya nchini wa Kongamano la kuwawezesha
Kiuchumi Wanawake, Wasichana na Wavulana dhidi ya Maambukizi ya Virusi
vya Ukimwi lililofanyika leo jijini Dar na kuratibiwa kwa pamoja kati ya
ILO na TACAIDS.
Washiriki wa Kongamano hilo wakiangalia baadhi ya machapisho mbalimbali ya VVU na Ukimwi.
Picha juu na chini mgeni rasmi katika
picha ya pamoja na washiriki wa Kongamano hilo la siku moja
lililofanyika jijini Dar es Salaam.
Comments