Kikosi cha kwanza cha Taifa Stars kilichoshuka dimbani juzi 
Thomas Ulimwengu akichuana na beki wa Morocco.
Sehemu ya mashabiki mbalimbali wa Taifa Stats waliokwea pipa mpaka morocco kwa lengo la kuipa nguvu wakishangilia
--
Taifa Stars imepoteza mechi ya ugenini baada ya kufungwa mabao 2-1. Mechi hiyo ya kundi C ya mchujo kuwania tiketi ya kucheza fainali za Kombe la Dunia mwakani nchini Brazil dhidi ya Morocco imechezwa usiku wa kumakia  jana kwenye uga wa Grand Stade de Marrakech, jijini Marrakech.

Licha ya kufungwa, Stars ndiyo iliyokuwa ya kwanza kumjaribu kipa wa Morocco, Nadir Lamyaghri aliyeokoa shuti la mpira wa adhabu la Aggrey Morris katika sekunde ya 40 tu tangu refa Daniel Frazier Bennett kutoka Afrika Kusini apulize filimbi ya kuanzisha pambano hilo.

Refa alitoa faulo hiyo baada ya mshambuliaji Thomas Ulimwengu kukwatuliwa na Ahmed Kantari baada ya kumtambuka beki mwingine wa Simba hao wa milima ya Atlas.

Stars walicheza pungufu kwa dakika 58 baada ya Morris kutolewa nje kwa kadi nyekundu kwa kumkwatua ndani ya eneo la hatari Abdelaziz Barrada huku akiwa amebaki yeye na mshambuliaji huyo. Adhabu hiyo iliandamana na penati ambayo Morocco waliitumia kupata bao la kuongoza dakika ya 37 mfungaji akiwa Abderazzak Hamed Allah.

Kabla, Stars wanaodhaminiwa na Kilimanjaro Premium Lager walitengeneza nafasi nzuri ya kufunga dakika ya 25 baada ya Ulimwengu kufanikiwa kuwatoka mabeki wawili wa Morocco na kuingia eneo la hatari lakini shuti lake hafifu lilidakwa na kipa Lamyaghri.

Morocco waliongeza bao lingine dakika ya 50 na Youssef El Arabi baada ya mabeki wa Stars kujichanganya katika kudhibiti pasi ya mwisho ya wachezaji wa timu hiyo, na mshambuliaji huyo kumfunga kirahisi kipa Juma Kaseja.

Kiungo mshambuliaji Amri Kiemba aliifungia Stars bao maridadi dakika ya 61 kwa mkwaju wa mbali uliomshinda kipa Lamyaghri. Kabla ya kuachia shuti hilo, Kiemba aliwatoka wachezaji wa timu ya Morocco ambayo ndiyo imepeta ushindi wake wa kwanza katika mechi hizo za mchujo za Kombe la Dunia.

Dakika sita kabla ya filimbi ya mwisho Mbwana Samata angeweza kuisawazishia Stars, lakini licha ya kuwatoka mabeki wawili wa Morocco baada ya kupokea pasi ya John Bocco mpira aliopiga ulitoka nje.

Stars ambayo bado inashika nafasi ya pili katika kundi hilo ikiwa na pointi sita inaondoka hapa kesho (Juni 9 mwaka huu) mchana kwa ndege ya EgyptAir kupitia Cairo, Misri na itawasili Uwanja wa Ndege wa Kimataifa wa Julius Nyerere (JNIA) saa 11 alifajiri (Juni 10 mwaka huu).

Mechi ilishuhudiwa na watanzania takriban 500 waliotoka Dar, waishio Morocco na nchi jirani wakiongozwa na Naibu Waziri wa Habari, Utamaduni na Michezo, Amos Makala.

Kamati ya Ushindi ya Taifa Stars pia iliwakilishwa na wajumbe kadhaa akiwemo Kaimu Mwenyekiti Ramadhan Dau, Mohamed Dewji na Zitto Kabwe.
 
Katika mechi hiyo Stars iliwakilishwa na; Juma Kaseja, Erasto Nyoni, Shomari Kapombe, Aggrey Morris, Kelvin Yondani, Frank Domayo, Mrisho Ngasa/Nadir Haroub, Salum Abubakar, Thomas Ulimwengu/Khamis Mcha/John Bocco, Amri Kiemba na Mbwana Samata. 

Taifa Stars inatarajiwa kurejea nyumbani leo Jumatatu saa kumi na moja na nusu alfajiri kwa ndege ya Shirika la Egypt Air.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*