SAFARI YA MWISHO YA MSANII ALBERT MANGWEHA YATIKISA DAR NA MOROGORO LEO

Maelfu ya wakazi wa jiji la Dar es Salaam na vitongoji vyake leo wameshiriki kuaga  mwili  wa  msanii mahiri wa muziki wa kizazi kipya, Albert Kenneth Mangweha 'Ngwair' aliyefariki dunia ghafla Mei 28 mwaka huu huko nchini Afrika Kusini. Mwili wa marehemu Mangweha kwa  sasa tayari umewasili mkoani Morogoro kwa mazishi yatakayofanyika kesho  huku  maelfu ya  wananchi  wa Morogoro wakiwa  wametanda barabara  kuaga mwili huo 


 
Ilikuwa ni simanzi kwawale hasa waliokuwa wakipata Burudani kutoka kwa Albert Mangwair na hakika aliyethibitisha kwa kuona kuwa sasa amelala na hainuki hadi Masiha atakapo rudi walishindwa kujizuia kwa vilio kama Rasta huyu kutoka Ukonga Mazizini maarufu kwajina la Simaga akitokwa na machozi baada ya kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa Marehemu Albert Mangwea katika viwanja vya Lidaz Kinondoni jijini Dar es Salaam. 
Mamia ya Wakazi wa jiji walijitokeza kumuaga Msanii huyo wa muziki wa kizazi kipya aliyefariki Mei 28, mwaka huu Nchini Afrika Kusini alikokuwa kwa shughuli za kimuziki. 
Mangwewa alisafirishwa mchana wa leo kwenda Kihonda mkoani Morogoro kwa mazishi yatakayo fanyika kesho.

Wasanii wa Bongo Movie wakipita kutoa heshima za mwisho kwa Mwili wa marehemu.
Wasananii wa muziki nao wakipita kutoa heshima za mwisho.
Hata wanahabari nao kama Issa Mnali walitoa heshima za mwisho.
Ras Simaga akipita na zana zake baada ya kutoa heshima za mwisho.
Miraji Kikwete akizungumza machache na Ummy Wenselaus 'Dokii' viwanja vya Lidaz
Juu ni wana Dar es Salaam wakiwa katika folenina chini watu wachache waliokuwa wameketi.
Wanafamilia wakiwa katika jukwaa lao.
Wadau wakubwa wa kazi za Ngwair wakiwa katika pozi la majonzi.
Wakazi wa jiji wakiwa na majonzi lakini FK Blog imebaini kuwa misiba ya wasanii hujaa watu wengi lakini si wote wanaenda kuomboleza bali wengine hufika kwaajili ya kuwaona 'LIVE' wasanii tofauti na walivyozoea katika luninga.
Kamati ya Maandalizi ya Mazishi ya Ngwair ikiwa jukwaani.(PICHA NA http://mrokim.blogspot.com

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*