Na meneja Mipango na Utafiti wa Sahara Media Group Ltd, Nathan
Lwehabura kwa niaba ya Uongozi, amewemgomea Nkoma wa TCRA;
Mei 23, 2013 Star Tv kupitia kwa mwanasheria wake
iliwataka Star-Time kuiondoa kwenye king’amuzi chao ifikapo saa 6:00 Usiku Mei
31, mwaka huu kutokana na kurusha na kuuza maudhui ya vipindi vyake bila idhini
na kukiuka sheria na haki za Hakimiliki.
Katika barua hiyo Star Tv iliwakumbusha Star-Time
hawakuwa na mkataba wa kurussha vipindi vya kituo hicho kwa mujibu wa sheria ya
Mawasiliano ya EPOCA na pia hawana haki ya kutumia maudhui ya yake bila idhini
yao chi ni ya sheria ya hakimiliki ya Tanzania na Kimataifa.
Mei 31 mwaka huu, Star-Time (Star Media) walijibu kwamba
hawajakiuka sheria yoyote na kusisitiza kwamba wataendelea kurusha matangazo
hayo kutekeleza matakwa ya Sheria ya EPOCA na sheria zake, na Juni 6 mwaka huu
Star TV iliwaandikia tena Star-Time na kusisitiza nia yake ya kuchukua hatua
zaidi kutokana na kuendelea kukaidi ombi hilo la kusitisha matangazo hayo na
kuainisha mapungufu kadhaa ya kisheia kwa upande wao yanayoifanya Star Tv
ijiondoe katika king’amuzi chao ifikapo Juni 8 mwaka huu.
Star Tv ilieleza Star Media inayomilikiwa kwa pamoja na
TBC na Star-Time kwamba inayo leseni ya miondo mbinu ya kurusha matangazo ya
Televishane ya kupitia mafumo wa (Multiplex Operator License DTT)
inayowaruhusu kuingia makubaliano ya Huduma na vituo mbalimbali kuwarushiwa
matangazo yao, lakini Star –Time hawana leseni ya kutoa huduma ya mahudhui
ambayo ni Content Service Provider License.
Star-Time ni kampuni ya kimataifa iliyoanzishwa China
inayotoa huduma za mahudhui katika nchi mbalimbali za afrika ikiwamo Tanzania
ili kupata mahudhui inalazimika kuingia mktaba na vituo vya Televisheni kabla ya
kuviingiza kwenye King’amuzi chake na baadaye kuuza mahudhui hayo kwa walaji
kwenye Mataifa hayo.
Star-Time inachukua vituo vya Televisheni bila idhini yao
na kuweka katika King’amuzi chake kwa kisingizio kamba wanaruhusiwa na sheria ya
EPOCA na kanuni zake, lakini sheria hiyo inasisitiza kuwapo kwa mkataba wa
makubaliano (SLA) kwa pande zote husika.
Kwa mujibu wa mahudhi
ya TV za Tanzania yanauzwa kwa walaji katika nchi nyingine kama Rwanda, Kenya,
Uganda, Burundi na Nigeria bila idhini ya wamiliki wake na kwamba wanaomiliki
mahudhui hazina uwezo wa kuidhibiti Star Time isirushe mahudhui yao nje ya nchi
ya Tanzania kwa kuwa baadhi ya mahudhui wanayonunua nje kama Tamthilia na
vipindi vinginevyo haviruhusiwi na watunzi au wasambazi wake kurushwa nje ya
nchi.
Lakini uhusiani wa makampuni haya mawili ya Star Media
(T) na Star-Time ya China yenye matawi mengi nchini Afrika katika
uendeshaji wa matangazo ya Dijitali haijabainisha vizuri ili kujua nani ni nani
na nini anachofanya hapa Tanzania katika misingi ya maelewano ya biashara, hivyo
kutokana na mantiki ya hoja hizo Star –Time waliiondoa mara moja Star TV kwenye
King’amuzi chao kama walivyoeolekewa na Star TV hiyo Juni 8.
Star Tv haioni sababu za kulazimishwa na TCRA kurushwa na
Star Time pasipo kuondoa hitilafu hizo za kisheria na bila kuangalia sheria
nyingine zinazolinda haki za TV huru kama sheria ya Hakimiliki na sheria za
Ushindani katika soko moja. TCRA kwa kutozingatia hili inataka kujifanya mmiliki
wa sheria hata zisizokuwa chini ya mamlaka yao..
Comments