TAARIFA ZA KIFO CHA MSANII SAIDA KAROLI NI UZUSHI MTUPU


Baada ya taarifa kuzushwa kuwa Mwanamuziki wa asili, Saida Karoli amefariki katika ajali ya meli habari za uhakika ni kuwa Saida Karoli wala hay uko mahala popote jirani na Ziwa Victoria. 
Baada ya kuweko Dar es Salaam wiki iliyopita, Saida na kundi lake walikodishwa na kuelekea Makongorosi Chunya mahala aliko mpaka asubuhi hii.
Saida Karoli anasema "sina mpango wowote wa kufa hivi karibuni". 
MUNGU AMUONGEZEE SIKU NYINGI ZENYE FARAJA KATIKA MAISHA YAKE
Source Sana na wasanii.chanzo  Juma Mtanda Blog

MSANII SAIDA KALOLE AZUSHIWA KIFO






Jana  kumekuwepo na taarifa kutoka kwa mwanahabari, Frederick Katulanda kupitia kundi pepe la majadiliano la MabadilikoTanzania, zikiipoti kuwa mwanamuziki aliyekuwa maarufu Tanzania na Afrika Mashariki, Saida Karoli, amefariki dunia  katika ajali ya kuzama kwa boti.

Kwamba, boti hiyo iliyokuwa ikisafiri kutoka katika kisiwa cha Goziba ilikumbwa na dhoruba ndani ya maji ya ziwa Nyanza (Victoria) na kusababisha kifo cha mwanamuziki huyo na watu wengine waliokuwa wakisafiri pamoja katika chombo hicho.

Taarifa ya Neville Meena imetoa angalizo kutafuta uhakika kwani inasemekana kuwa Saida Karoli ni mzima, yupo jijini Dar es Salaam na hajafariki dunia kama inavyoelezwa: “Nimetafuta namba yake ya simu sijaipata, ila taarifa kutoka Bukoba na ofisi ya Ofisa Utamaduni Muleba zinasema siyo kweli... kulikuwa na uvumi mwingi mjini Bukoba na Wilayani Muleba kuhusu mwanamuziki huyo kufariki lakini baadaye ikathibitika kwamba hakuwa mmoja wa abiria.” ameandika Meena.

Kuhusiana na ajali ya boti, Meena amesema, “...ni kweli kwamba kuna boti imezama katika Ziwa Victoria.”ila  msanii  huyo hakuwepo katika  boti  hiyo na  wala hayupo  wilayani Muleba hivyo  taarifa  hizo  hazina  ukweli wowote na mtandao  huu unamwombea maisha marefu  zaidi msanii Saida Kalole

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.