TARATIBU ZA KUUAGA MWILI WA KATIBU MKUU KIONGOZI WA ZAMANI MAREHEMU TIMOTH APIYO



 THE UNITED REPUBLIC OF TANZANIA
DIRECTORATE OF PRESIDENTIAL COMMUNICATIONS

Telephone: 255-22-2114512, 2116898
              press@ikulu.go.tz             

Fax: 255-22-2113425


Coat of Arms
PRESIDENT’S OFFICE,
      THE STATE HOUSE,
              P.O. BOX 9120,  
DAR ES SALAAM.
Tanzania.
 

TAARIFA KWA VYOMBO VYA HABARI
Ndugu Wahariri, tunapenda kuwataarifu kuwa mwili wa Marehemu Mzee Timothy Apiyo (Katibu Mkuu Kiongozi Mstaafu), aliyefariki siku ya Jumatatu 10, Juni 2013 katika Hospitali ya Millpark, Johannesburg, Afrika Kusini, utawasili katika uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere – DSM kesho, Ijumaa 14 Juni, 2013 saa moja usiku. Baada ya kupokelewa mwili utapelekwa nyumbani kwake Ukonga Sitakishari ambako mwili utalala hapo.
Shughuli za kuaga mwili wa Marehemu Mzee Timothy Apiyo zitafanyika siku ya Jumamosi 15, Juni 2013 katika viwanja vya KARIMJEE kuanzia saa 2.00 asubuhi hadi saa 4.00 asubuhi.
Baada ya hapo mwili wa marehemu Mzee Timothy Apiyo utapelekwa uwanja wa ndege wa Mwalimu Julius Nyerere tayari kwa safari ya kwenda Rorya kwa ajili ya mazishi.
Tunaomba ushirikiano wenu.
“ASANTENI”
Imetolewa na:
Kurugenzi ya Mawasiliano ya Rais,
Ikulu.
Dar es Salaam.
13 Juni, 2013

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.