Umoja wa Watanzania Ujerumani (U.T.U ) Kushiriki katika Festival ya "BrΓΌderschaft der vΓΆlker " mjini Aschaffenburg " Ujerumani litakaloanza Julai 19 hadi 21, 2013

Mhe. Mfundo, Mwenyekiti wa UTU.
Watayarishaji wa Festival ya "BrΓΌderschaft der vΓΆlker " mjini Aschaffenburg, nchini Ujerumani wameuhalika Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kushiriki katika maonyesho hayo utamaduni wa nchi mbali mbali yatakayoanza 19 hadi 21 Julai 2013.

Watayarishaji wa maonyesho hayo wamevutiwa sana na shughuli za Umoja wa Watanzania Ujerumani (UTU) kwa juhudi zake za kuitangaza Tanzania.

Wandaaji hao, wametoa nafasi kwa umoja wa watanzania kushiriki na kuitangaza Tanzania kwa kasi zaidi.

Mwenyekiti wa UTU, Bw. Mfundo Peter Mfundo ameupokea mwaliko huo kwa mikono miwili na amewaomba Watanzania wote wanaoishi Ujerumani kujitokeza kwa wingi katika maonyesho hayo na kuitumia nafasi waliyopewa kwa maslahi ya Tanzania na Watanzania ambapo Umoja wa Watanzania (UTU) utakuwa na banda lake katika maonyesho hayo.

Mnakaribishwa wote na kwa maelezo zaidi wasiliana na kamati.utu@googlemail.com pia unaweza kutembelea link ya maonyesho at http://www.bruederschaft-der-voelker.de/2013/05/29/union-of-tanzanians-in-germany/

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.