UNAFIKIRI NI KWA NINI NYERERE ALIPINGA SERIKALI TATU?

Rasimu ya Katiba iliyotolewa hivi karibuni na Tume ya Katiba imetoa mapendekezo ya kuwepo kwa Muungano wa Serikali Tatu.
Kwa mujibu wa Mwenyekiti wa Tume hiyo, Jaji Joseph Warioba, Serikali ya Muungano iliyokuwa ikisimamia mambo 22 sasa itabaki na mambo saba, huku mengine yakirudishwa kwenye Serikali za Zanzibar na Tanzania Bara.
Amedokeza kuwa mbali na Serikali tatu, wapo wananchi waliotaka Serikali moja, mbili, nne na wengine Muungano wa Mkataba.
Kwa maoni yangu Tume ya Katiba imethubutu kusikiliza kilio cha wengi waliokuwa wakiukosoa Muungano. Ni jambo ambalo Chama Cha Mapinduzi hakikupenda kuvunja mwiko, ndiyo maana kinasisitiza Serikali Mbili.
Mimi naamini kabisa, kwa jinsi Mwalimu Nyerere alivyokuwa na misimamo yake, angekuwa hai leo, asingekubaliana na rasimu hii ya Katiba.
Asingekubali kuona Muungano aliouasisi ukiwa hatarini kuvunjwa kwa kuwaridhisha wanaotaka Serikali Tatu.
Tukiangalia chanzo cha Muungano wetu, utaona sababu nyingi, lakini ya msingi ni ya usalama. Ni kweli kuna wanaosema watu wa Tanganyika na Zanzibar wana undugu, lakini hii haina mashiko kwani hata ukiangalia nchi zote zilizotuzunguka tuna undugu kwa njia moja au nyingine, mbona hatuungani?
Wengine wanahusisha Muungano na vita baridi kati ya Urusi na Marekani miaka ya 1980. Inawezekana, lakini mbona vita hiyo ilipoisha Muungano huo haukuvunjika.
Kwa hiyo, sababu kubwa Muungano wetu ni usalama. Baada ya kupata uhuru mwaka 1961, Mwalimu Nyerere kama viongozi wengine wa Afrika walitafuta njia za kulinda mamlaka yao kwa namna yoyote ile.
Kwa Nyerere, Zanzibar ilikuwa tishio siyo la utawala wake tu, bali kwa Tanganyika nzima. Ndiyo maana aliwahi kukaririwa akisema, angetamani Tanganyika ivimeze visiwa hivyo au avisogeze mbali kabisa na eneo lake.
Kumbuka wakati huo tayari kulikuwa na chokochoko za kisiasa zilizoanza tangu miaka ya 1957 kati ya vyama vya ASP, ZNP, ZPPP na Umma.
Mwalimu alihofu kuwa vurugu hizo zingeambukiza wanasiasa wa bara au hata maadui wa nje kuvitumia visiwa hivyo kushambulia Tanganyika.

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.