Wandishi wa Habari Mkoani Mbeya wametakiwa kuisaidia jamii kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na Watoto uliokithiri vitendo ambvyo hupelekea kuwa na ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.


Mwezeshaji kutoka Walter Reed Program Hijja Wazee wakati akitoa Semina kwa waandishi wa Habari 20 iliyofanyika katika ukumbi wa Youth Centre wa Kanisa Katoliki uliopo Jijini Mbeya.


Mwezeshaji kutoka Walter Reed Program Mergitu Ebba akiwanoa waandishi wahabari waliohudhuria semina hiyo



Baadhi ya waandishi wa habari wakiwa makini kumsikiliza mwezeshaji






Wandishi wa Habari Mkoani Mbeya wametakiwa kuisaidia jamii kupinga vitendo vya unyanyasaji wa kijinsia na Watoto  uliokithiri vitendo ambvyo hupelekea kuwa na ongezeko la maambukizi ya Virusi vya Ukimwi.
Kauli hiyo imetolewa na Mwezeshaji kutoka Walter Reed Program Hijja Wazee wakati akitoa Semina kwa waandishi wa Habari 20 iliyofanyika katika ukumbi wa Youth Centre wa Kanisa Katoliki uliopo Jijini Mbeya.
Mkufunzi huyo amesema kukithiri kwa vitendo vya unyanyasaji wa Kijinsia ndani ya jamii vinaweza kumalizwa endapo Wanahabari watafanya kazi ya kujitolea ya kuibua na kuiambia jamii madhara ya vitendo hivyo.
Ameongeza kuwa zaidi ya asilimia 60 ya jamii ya Mbeya inasadikika kujihusisha na vitendo vya ukatili wa kijinsia na kwamba Mfuko wa raisi wa Marekani umetoa fedha kwa ajili ya kuhakikisha Vitendo hivyo vinaisha ambapo msaada huo utalenga Nchi tatu ikiwemo Tanzania.
Amesema Nchini Tanzania ni Mikoa minne  itakayohusika  ambayo ni Mbeya, Iringa, Mara na Dar Es Salaam ambapo kwa Mkoa wa Mbeya ni Wilaya Sita zitakazohusika ambazo ni Mbeya Jiji, Ileje, Kyela, Rungwe, Busokelo na Mbeya Vijijini.
Na Mbeya yetu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA