ABILIA ZAIDI YA 50 WANUSURIKA KUFA BAADA KUTOKEA AJALI YA BASI LA PRINCESS MURO KUWAKA MOTO NZEGA TABORA.



ABIRIA zaidi ya 50 wilayani Nzega mkoani Tabora wamenusurika kupoteza maisha baada ya basi walilokuwa wakisafiria kuungua moto kutokana na hitilafu ya kiufundi.

Kamanda wa Polisi wa Mkoa wa Tabora, Peter Ouma alisema moto huo ulioteketeza mizigo yote ya abiria, ulitokea juzi saa 4 usiku katika kijiji cha Nata kwenye basi la Princess Muro.

Alisema gari hilo aina ya Scania lenye namba za usajili T 6766 CEH, lilikuwa likitoka Dar es Salaam kwenda Mwanza likiwa linaendesh
wa na dereva Boniface Francis.

Alisema likiwa na mwendo wa kawaida, lilianza kuwaka moto ndipo kondakta pamoja na dereva waligundua na kulisimamisha.

Abiria walifanikiwa kushuka wakiwa salama isipokuwa mizigo yao iliteketea kwa moto. Jitihada za kuuzima zilishindikana kutokana na eneo ilikotokea ajali hiyo kukosa kikosi cha zima moto na uokozi.

Kwa mujibu wa kamanda, kulitokea hitilafu kwenye injini ya gari hilo hali iliyosababisha moto. Hakuna mtu alijeruhiwa.

Kamanda amewataka wamiliki wa vyombo vya usafiri hususani vya kusafirisha abiria, kufanya ukaguzi na kuvikarabati kwa nyakati tofauti kuepusha ajali.
chanzo:manalony

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

DKT NCHIMBI AWAAHIDI MAKUBWA WANANCHI WA KWELA, RUKWA

DKT NCHIMBI ASHIRIKI MAZISHI YA ASKOFU.GACHUMA WA KANISA LA NLGCC

π™‚π˜Όπ™ˆπ™Šπ™‰π˜Ώπ™„ π™†π˜Όπ˜Ύπ™ƒπ™€π™•π˜Ό π™†π™„π˜½π™„π™‰π™‚π™’π˜Ό.