AIBU! JIJI LA MBEYA LAVAMIWA NA MABANGO YA WAGANGA WA JADI.

JE TANESCO MNALIONA HILI NA MNALIPWA KUPITIA TANGAZOZ HILI?
 WAKATI JIJI LIKIWA LIMEFANYA  JUHUDI KUBWA LA KUPANDA  MITI NA KUITUNZA WAGANGA WAMEANZA  KUHARIBU KWA KUPIGA MISUMARI
 MITI HII HUCHUKUA TAKRIBANI MIAKA 10 KUFIKIA ILIPO FIKIA HAPA LAKINI WAGANGA BILA HURUMA WANAISHINDILIA NA MISUMARI
TAYARI MTI HUU UMEANZA KUHARIBIKA KWA KUKOSA MATUNZO
  JE WATOZA USHURU WA MABANGO YA JIJI MNAYAONA HAYA ?
 MGAMBO WA JIJI MNAFANYA KAZI GANI? 
 MWENYEKITI WA TIBA ASILI MKOA WA MBEYA JE UMEYARUHUSU HAYA ?
NAFASI INAGOMBEWA BAINA YA MACHINGA NA MGANGA
 MCHUNGAJI MWAMALANGA AMBAYE WEWE NI MDAU WA MAZINGIRA UNAYAONA HAYA?  


 BANGO HILI LIMEBANDIKWA KWENYE NYUMBA YA MTU JE LINALIPIWA KODI?
**
Wakati halmashauri ya Jiji la Mbeya ikifanya kila juhudi kuimarisha miundombinu ya barabara zake kwa kuweka lami na kupanda miti lakini imekuwa kinyume kwa baadhi ya watu ambao wamekuwa mstari wa mbele kukwamisha juhudi hizo.

Hayo yamebainishwa na mtando huu baada ya kutembelea maeneo kadhaa na kukuta uharibifu mkubwa wa miti ambayo imepandwa kandokando ya barabara zinazo ingia Kati Kati ya Jiji ,athari kubwa imeanza kuonekana kuanzia eneo la Sae Hadi kati kati ya jiji. 

Baadhi ya watu ambao   wamekuwa mstari wa mbele kuchafua mandhari ya jiji kwa kubandika mabango yao wakati ungozi wa chama cha tiba asili na tiba mbadala kupiga marufuku kubandikwa mabango haya barabarani .

Wengine wanaochangia kuharibu Mandhari hiyo ni wamiriki wa vibanda vya kutolea fedha ambavyo vimetapakaa jiji zima na kufanya jiji kuwa kama kijiji cha ujamaa na kuzifanya asasi za Mabenki kubaki hazina fedha huku pesa zikimilikiwa mitaani na hivyo kuna hatari mzunguko wa fedha bandia kuingia katika uchumi kwani watu wengi hawana vifaa vya kutambua fedha bandia.

Hata hivyo uchunguzi wa  mtandao huu umebaini kwamba viongozi wa siasa wamekuwa mstari wa mbele kuchochea uchafu huo kwa kuto wambia ukweli wapiga kura wao hivyo yakitokea Magonjwa Ya mripuko ni Serikali inayo ingia gharama kubwa za matibabu hali ambayo ingeweza kuepukika 


Mtandao huu umebahatika kutembelea miji mingi na kubaini kwamba vibanda hivyo vimekuwa ndani ya maduka na barabara zikiwa salama na kuondoa adha kwa watumiaji wa barabara na kuwa hatari kusababisha ajali.

ILI KUSAFISHA JIJI HILI NANI AMFUNGE PAKA KEGERE NA NANI WA KULAUMIWA, MWANANCHI, HALMASHAURI AU VIONGOZI WA SIASA ?
Na Mbeya yetu

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*