ARSENAL YAENDELEZA MAUWAJI, YAWAFUMUA 7-1 WAVIETNAM LEO
IMEWEKWA
JULAI 17, 2013 SAA 5:00 USIKU
ARSENAL imeendeleza wimbi la ushindi mnono katika mechi
za kujiandaa na msimu, baada ya leo kuifumua mabao 7-1 Vietnam XI kwenye Uwanja
wa My Dinh mjini Hanoi.
Ushindi huo umemoa majibu kadhaa kocha Arsene Wenger,
kwanza kama atashindwa kusajili mshambuliaji wa kiwango cha dunia kabla ya mechi
ya ufunguzi ya Ligi Kuu England dhidi ya Aston Villa, Olivier Giroud atatosha
kwenye kampeni ya ushindi baada ya leo kufunga mabao matatu peke
yake.
Pili, anaweza kumtumia Bacary Sagna katika beki ya kati
itakapotokea dharula kama atakwama kumsajili beki wa Swansea, Ashley Williams
baada ya beki huyo kulia wa Arsenal kucheza namba nzuri leo.
Na tatu, inayoweza kuwa muhimu kuliko zote, Jack
Wilshere na kama yuko fiti kabisa kuanza msimu, baada ya kucheza mechi yake ya
kwanza leo tangu afanyiwe upasuaji wa kifundo cha mguu Mei.
Shukrani! Wachezaji wa Arsenal
wakiwa wamebeba bango la 'Asanteni' kwa ajili ya mashabiki baada ya kuwafunga
Vietnam
Shughuli: Beki wa Arsenal,
Bacary Sagna akiupitia mpira miguuni mwa Nguyen Anh Duc wa Vietnam
Mbali na mabao matatu ya
Giroud, mabao mengine ya Arsenal leo yamefungwa na Alex Oxlade-Chamberlain,
Chuba Akpom mawili na Ignasi Miquel ambao wote walifunga pia kwenye ushindi wa
7-0 katika mchezo wa kwanza dhidi ya Dream Team ya Indonesia.
Kikosi cha Arsenal leo
kilikuwa; Szczesny/Martinez dk71, Sagna/Aneke dk71, Jenkinson/Olsson dk71,
Koscielny/Mertesacker dk46, Gibbs/Miquel dk46, Arteta (Nahodha)/Ramsey dk46,
Rosicky/Zelalem dk46, Oxlade-Chamberlain/Wilshere dk66, Gnabry/Walcott dk46,
Podolski/Miyaichi dk46 na Giroud/Akpom dk46
Olivier Giroud akifunga moja
ya mabao yake leo
Chuba Akpom akishangilia bao
lake na mchezaji mwenzake, Alex Oxlade-Chamberlain
Giroud akifanya
safari
Chuba Akpom akishangilia bao
lake leo
Serge Gnabry akipasua ngome ya
Vietnam
Alex Oxlade-Chamberlain pia
alifunga leo
RATIBA YA MECHI ZA ARSENAL KUJIANDAA NA MSIMU
Julai 14 na Indonesia XI walishinda 7-0
Julai 17 na Vietnam wameshinda 7-1
Julai 22 na Nagoya Grampus (Uwanja wa Toyota, Japan) Saa 5.30 asubuhi
Julai 26 na Urawa Red Diamonds (Uwanja wa Saitama, Japan - Kombe la Saitama City) Saa 5.30 asubuhi
Agosti 3 na Napoli (Kombe la Emirates) Saa 10.20 jioni
Agosti 4 na Galatasaray (Kombe la Emirates) Saa 10.20 jioni
Agosti 10 na Manchester City (Uwanja wa Olimpiki, Helsinki) Saa 9 jioni
Julai 17 na Vietnam wameshinda 7-1
Julai 22 na Nagoya Grampus (Uwanja wa Toyota, Japan) Saa 5.30 asubuhi
Julai 26 na Urawa Red Diamonds (Uwanja wa Saitama, Japan - Kombe la Saitama City) Saa 5.30 asubuhi
Agosti 3 na Napoli (Kombe la Emirates) Saa 10.20 jioni
Agosti 4 na Galatasaray (Kombe la Emirates) Saa 10.20 jioni
Agosti 10 na Manchester City (Uwanja wa Olimpiki, Helsinki) Saa 9 jioni
Comments