DC Ilala awaomba wadau kuwekeza katika mpira wa miguu

Mkuu wa Wilaya ya Ilala Raymond Mushi akikabidhi kombe kwa nahodha wa timu ya Stakishali waliokuwa mabingwa katika fainali ya Diwani Bonnah Cup iliyochezwa jana. Katikati ni Diwani wa kata ya Kipawa Mh. Bonnah Kaluwa. Stakishali waliokuwa mabingwa walipata shs laki tano pamoja na kombe.
*************
Na Mwandishi Wetu
MKUU wa wilaya ya Ilala Raymond Mushi amewasisitiza wadau mbali mbali kuwekeza katika mpira wa miguu kwani hutoa ajira nyingi kwa vijana na kuwafanya wajipatie kipato.

Akiongea na waandishi wa habari baada ya kufunga mashindano ya Bonnah Cup yaliyoandaliwa na diwani wa kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa, Mkuu wa wilaya alisema kuwa kwa miaka ya sasa mpira umekuwa kimbilo kubwa la ajira kwa vijana kwani huweza kuwasaidia kujiingizia kipato.

Mushi alisema kuwa pamoja na wadau kuwekeza katika mpira wa miguu, Tanzania itaweza vile vile kukuza vipaji ambavyo huwa vinapotea.
“Tanzania tuna vipaji vingi sana vya mpira wa miguu, tatizo ni vipaji hivyo kuvumbuliwa hivyo nawaombeni wadau mbali mbali kutoka sekta zote kujitokeza kuweza kuwekeza katika tasnia hii, ambapo tutawezesha vijana wetu kujipatia ajira,” alisema.
Timu ya Stakishari kutoka Mogo iliifunga timu ya Vipaji Halisi kutoka eneo la airport katika fainili na kukabidiwa kombe pamoja na kiasi cha shilingi laki tano, ambapo mshindi wa pili alipata kiasi cha shilingi laki tatu na mpira moja na mshindi wa tatu alipata shilingi laki moja na mpia.
Jumla ya timu 20 kutoka katika kata ya kipawa zilishiriki katika mashindano hayo.
Muandaaji wa mashindano hayo diwani wa kata ya Kipawa Bonnah Kaluwa alisema “Lengo kubwa ya kuandaa mashindano haya ni kuwaleta vijana pamoja iliwaweze kufahamiana na kushirikiana lakini pia kuinua vipaji vya vijana katika mchezo wa mpira wa miguu.
Vijana wengi wanaocheze katika ligi hapa nchini wamechipukia katika kata ya Kipawa. “ Napenda kuendeleza na kukuza vipaji wa vijana iliwaweze kufikia kiwango cha juu zaidi katika mchezo huu”, alisema
Said Mkuwa, Mwenyekiti wa mashindano hayo aliongezea: “Tunamshukuru sana diwani kuandaa mashindano haya kwa ajili ya vijana, alisema Nimefurahi kwamba mashindano yamekwenda vizuri tangu mechi za mwanzo hadi fainali na vijana wameshirikiana vizuri katika michezo yote” 

Comments

HABARI ZILIZOSOMWA ZAIDI

MAKABILA 10 YENYE WANAWAKE WAREMBO TANZANIA

NI SIMBA PEKEE ILIYOFUNGWA ROBO FAINALI

CHATANDA AFUNGUA MAFUNZO YA KUWAJENGEA UWEZO MADIWANI WANAWAKE WA MIKOA 11

KINANA ASIMIKWA KUWA MMOJA WA MACHIFU WA WAPARE, SAME MAGHARIBI

DK NCHIMBI AMTEMBELEA MZEE YUSUF MAKAMBA*

AZIZ KI AAHIDI KILA ATAKAYEIFUNGA MAMELODI

HATUTOPAKI BASI DHIDI YA YANGA-MOKWENA

“PEMBA SALUTI KWENU” DK. NCHIMBI*